Zaidi ya wanafuni Elfu 50 wa Shule za Msingi katika Manispaa ya Sumbawanga wanatarajiwa kupatia dawa Kinga Tiba za minyoo kwaaajili ya kukabiliana na magonjwa ya homa za matumbo.
Dawa hizo ambazo zimeanza kutolewa leo inashirikisha Kata 15 zenye shule za Msingi 61 ambapo ambapo kata baadhi ya kata hazitahusika na zoezi hilo.
Kwa mujibu wa Mratibu wa magonjwa yasipatiwa kipaumbele wa Manispaa ya Sumbawanga Veronica Seleman kata ambazo hazitahusika ni zile ambazo tathimini ya zoezi hilo kwa mwaka uliopita zijaonesha kuwa kiwango cha maambukizi kwa wanafunzi kipo chini ya asilimia moja.
“Manispaa ina jumla ya shule za Msingi 71, lakini kuna baadhi ya kata hazihusihiwi baada ya kuona maradhi hayo yamepungua sana tofauti na miaka iliyopita na haya ni mafanikio makubwa kwetu,” alisema Veronica
Kaimu Afisa Elimu Msingi katika Manispaa hiyo Graceana Kilenga amesema kufanyika kwa zoezi hilo kumesaidia sana kupunguza utoro shuleni kutokana na wananfunzi wengi kutosumbuliwa na maradhi.
“Zamani ulikuwa unaweza kumwona mwanafunzi akitembea akiwa na tumbo kubwa ukadhani ni unene, kumbe anasumbuliwa na maradhi ya homa ya tumbo, japokuwa hivi sasa huwezi ukaona tatizo hilo, hii ni kutokana na kutolewa kwa dawa za Kinga Tiba.” Alisema Kilenga.
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa