Na Sammy Kisika.
Wakazi wa mkoa wa Rukwa wanaoishi ndani nje ya mkoa huo wametakiwa kuungana katika kuhakikisha mkoa huo unakuwa na umoja na unapata maendeleo kama lilivyokusudio la Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Akizungumza katika hafla ya kuliombea Taifa amani na Iftar maaalum iliyoandaliwa na mkoa kwa kushirikiana na Mdau wa maendeleo Jacquline Mzindakaya, Mgeni Rasmi katika shughuli hiyo Mkuu wa mkoa wa Rukwa Makongoro Nyerere amesema wakati mkoa ukitafakari mafanikio ya miaka minne ya serikali ya awamu ya Sita ya Rais Samia ipo haja pia ya kuona michango ya maendeleo ya Wanarukwa.
Makongoro alisema maendeleo yanahitaji ushirikiano wa pamoja kati ya wananchi na serikali na kuwataka Wanarukwa kuiga mfano wa Jacquline Mzindakaya ambaye amekuwa akitumia sehemu ya kipato chake na kusaidia jamii ya Wanarukwa kama alivyofanya kwa kuandaa futari hiyo kwa waumini wa Kiislamu na Kikristu ambao wako kwenye mfungo wa Ramadhan na Kwaresma.
Alisema katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Samia kuna mafanikio mengi yaliyopatikana kwenye sekta ya kielimu, afya, maji, miundombinu na mambo mengi ambayo yamelifanya Taifa kuwa na mabadiliko makubwa ya kimaendeleo.
Kwa upande wake Sheikh wa mkoa wa Rukwa Rashid Akilimali alisema ili maendeleo ya mkoa yaweze kupatikana ni lazima wakazi wa ndani na nchi ya nje ya mkoa wazungumze lugha moja na kuwataka baadhi ya viongozi wa Rukwa wakiwapo Wabunge kuacha kuwatenga viongozi wa dini katika mipango yao ya maendeleo.
Mdau huyo wa maendeleo Jacquline Mzindakaya alisema amekuwa na utaratibu wa kukutana na makundi mbalimbali ya jamii ya walemavu, wanawake na watu wengine kwa kula chakula pamoja lakini kutoa misaada katika sekta mbalimbali ikiwapo sekta ya afya.
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa