Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga anawatangazia Wananchi wote waliochukua Viwanja na kushindwa kulipia kwa muda mrefu katika Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga kuwa ametoa siku siku 30 kuanzia tarehe 01/07/2025 hadi tarehe 30/07/2025 ili kukamilisha malipo yote kwa watu wanaodaiwa Viwanja hivyo.
Mara baada ya siku 30 zilizotolewa kukamilika Halmashauri itafuta majina ya wahusika walioshindwa kukamilisha malipo yote ya Viwanja na kuvitangaza upya kwa wananchi wengine wenye uhitaji wa Viwanja hivyo.
Orodha ya majina ya Wananchi wanaodaiwa na Halmashauri ambao wanatakiwa kulipia haraka kabla ya kunyang'anywa Viwanja husika imeambatanishwa.
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa