Na Sammy Kisika, Kitengo cha Mawasiliano SMC
Mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga Pendo Mangali amewataka viongozi wa serikaliza mitaa waliochaguliwa hivi karibuni kwenda kutimiza wajibu wao kwa kuondoa kero za wananchi na wasiwe madalali wa kuchangia kuhujumu mapato ya halmashauri.
Katika hafla ya uapishaji viongozi hao wa serikali katika ngazi ya mitaa, vitongoji na vijiji Mkurugenzi Mangali aliwaasa kuwa wanapaswa kuwa msaada kwa serikali katika kushughulikia changamoto za wananchi na sio kuwa kikwazo kwa haki zao.
“ Mnaapishwa hapa hii leo nendeni mkachape kazi kwa kushirikiana na ofisi ya Mkurugenzi na msiende kuwa vinara wa kuuza viwanja na mashanba ya watu pasipo kufuata taratibu kiasi cha kutengeneza migogoro mingi ya ardhi, hiyo sihitaji kusikia”alisema Mangali.
Alisema yapo matarajio ambayo serikali inatamani kuona yanatekelezwa kuanzia ngazi za chini na wao ni tochi ya mipango ya maendeleo kuanzia kwenye mitaa na vijiji vyao, hivyo wanapaswa kuanisha ni mambo yepi ya maendeleo yanatakiwa kufanyika ili bajeti ya serikalu iweze kuchakatwa kuanzia ngazi ya chini.
Mkurugenzi huyo aliwataka viongozi hao kuzingatia viapo vyao na kutumia vibaya nafasi za kujinufaisha kinyume na taratibu kwasababu ya mihuri waliyokabidhiwa na ikatumika vibaya.
Alisema…”Sitaraji kuona mnatumia vibaya mihuri mliyokabidhiwa, twendeni tukawatumikia wananchi kwa mujibu wa viapo vyenu na uzuri ni kuwa ukikiuka kiapo unaweza kutenguliwa,wahudumieni wananchi kwa usawa na haki”.
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa