Waziri wa Ardhi Jerry Slaa hii leo anatarajiwa kwenda kwenye kijiji cha Sikaungu wilayani Sumbawanga kwaajili ya kumaliza mgogoro baina wa wakazi wa kijiji hicho na Mwekezaji wa shamba la Efatha.
Ziara ya Waziri huyo inakuja baada ya mwishoni mwajuma lililopita kufika kijijini hapo kuwasikiliza wananchi na kisha kuunda Kamati ambayo inatakiwa kuwasilisha ripoti yake hii leo kwa lengo la kumaliza mgogoro huo.
Mgogoro wa wananchi hao wa Sikaungu moja kijiji kinachopakana na shamba la Efatha ulianza mara baada ya shamba hilo ambalo lilikuwa la serikali chini ya DAFCO kabla ya kutangazwa kuuzwa mnamo mwaka 2006 na kununuliwa na Efatha ilihali kukiwa na kutofautiana mitazamo juu ya mipaka ya shamba hilo baina Mwekezaji na wakazi wa kijiji hicho.
Shamba la Efatha lenye ukubwa wa zaidi ya Hekta Elfu kumi linapakana kwenye halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga na ile halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga ambayo limo kwenye vijiji vya Sikaungu, Songambele na Msandamuungano
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa