Watoto wanaolelewa kwenye kituo cha Watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu cha Berthania Future anda Hope Centre cha mjini Sumbawanga wameishukuru serikali kwa kuwajali katika kipindi hiki cha Sikukuu ya Eid ambapo walishrerehekea vizuri kutokana na msaada wa vitu mbalimbali walivyopatiwa.
Furaha ya watoto na wafanyakazi wa kituo hicho inatokana na msaada wa vitu mbalimbali wakiwapo Mbuzi wawili, vyakula na vifaa vingine.
Akizungumzia msaada huo Mkuu wa kituo hicho Joseph Kasaila alisema kuwa kitendo cha kuolewa kwa msaada huo kinaonesha namna gani serikali inajali kundi hilo lakini pia kazi kubwa inayofanya na walezi hao kwa kulea watoto waoishi katika mazingira yao.
Alisema tangia kuanza kwa kituo hicho takribani miaka 20 sasa kimefanikiwa kuwalea watoto zaidi ya 2,500 ambao baadhi yao wamefanikiwa kubadilika tabia kiasi cha kupata ajira serikali na kampuni binafsi baada ya kusomeshwa kwenye vyuo mbalimbali.
Kasaila alisema kwa sasa wana watoto 68 ambao wanalelewa kituo hapo huku msaada mkubwa ukiwa ni kutoka kwa Wafadhili wao kutoka Ulaya ambao huchangia asilimia 70 ya bajeti yao ambayo ni Shilingi Milioni 200 kwa mwaka, huku asilimia 30 ikitakiwa kutolewa na jamii inayozunguka kituo hicho.
Akikabidhi msaada huo Mkuu wa wilaya ya Sumbawanga, Sebastian Waryuba alisema kuwa serikali inajali watu wake na ndio maana Waziri Mkuu ametoa misaada hiyo ili kundi hilo la watoto lipate kujisikia kuwa inawajali na kuwathamini.
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa