Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto imetoa miezi mitatu kwa Wakurugezni wa halmashauri zote nchini kuhakikikisha wanatoa mikoipo inayokidhi vigezo vya kibaiashara kwa makundi ya wanawake waliopo kwenye maeneo yao.
Wito huo umetolewa Waziri mwenye dhamana na wizara hiyo Mh.Ummy Mwalimu katika kilele cha maazimisho ya Siku ya wanawake Duniani kilichofanyika kwenye uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga mkoani Rukwa.
Waziri Mwalimu alisema wapo baadhi ya Wakurugenzi wanaopuuzia kutoa mikopo hiyo ihali wakifahamu kuwa serikali ilipita na kutoa ahadi kwa wanawake kuwa itawezesha kiuchumi kwa kuwapa mikopo hiyo ambayo inatokana na mapato ya ndani ya halmashauri.
"Mimi kama Waziri mwenye dhamana nasubiri hadi Juni 30, mwaka huu na iwapo kutakuwa na Mkurugenzi ambaye hatatoa mikopo kwa wanawake kwenye eneo lake basi ntachukua majina yao na kuyapeleka kwa Mheshimiwa Rais John Magufuli ili aweze kuwachukulia hatua za kupuuza agizo hilo".Alisema Waziri huyo
Aidha Waziri Mwalimu alikemea tabia ya baadhi ya Wakurugenzi ambao wamekuwa wakitoa mikopo kiduchu kwa wanawake, kiasi kwamba inawawia vigumu kufanya biashara walizokusudia.
Alisema..."Utakuta Mkurugenzi anatoa mkopo wa kiasi cha Shilingi Laki Tatu kwa kundi la wanawake sita , eti ili wagawane kila mtu shilingi Elfu hamsini, hivi Elfu hamsini unaweza kufanya biashara gani jamani? Na ndio maana hiyo mikopo wakitoa inashindwa kurejeshwa kwasababu hao wanawake wanaamua kuzitumia kwa matumizi mengineyo fedha hizo."
Alisema mikopo inayotolewa lazima ilenge kumwezesha mwanamke kujikwamua kiuchumi na kuendana na hali halisi ya uchumi wa viwanda ambapo mkakati uliopo unalenga sana katika kumwezesha mwanamke aliyepo vijijini.
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa