Halmashauri nchini zimetakiwa kubuni vyanzo vipya vya mapato ambavyo vitaunganishwa na mfumo mpya wa TAUSI katika ukusanyaji sahihi na uwekaji kumbukumbu wa mapato yote kwa mwaka.
Akizungumza wakati wa mafunzo kwa Wataalamu wa Idara ya Ardhi, Idara ya Fedha sanjari na Watendaji wa Kata na Vijiji wa Manispaa ya Sumbawanga, Afisa Kiongozi wa TEHAMA kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Rahabu Nyeneu aliwataka Wataalamu hao kujiandaa kwa kukusanya mapato ya majengo na mabango ambayo serikali imerejesha kwa halmashauri kukusanya kodi hiyo.
Nyeneu alisema kodi hiyo inaangukia katika sheria ya Fedha ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa , Sura ya 290 (2) iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2023, ambapo mabadiliko yameelekeza kuwa jukumu la kusimamia na kukusanya kodi ya majengo pamoja na ushuru wa mabango kuwa jukumu la serikali za mitaa ili kuziongezea wigo wa mapato halmashauri hizo.
KJwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga Kulanga Kanyanga amesema uwepo wa mafunzo hayo ni hatua nzuri kwa serikali kwa halmashauri ili kuleta tija katika ukusanyaji wa mapato hato ambayo yataongeza wigo wa kuihudumia jamii kwenye halmashauri na Taifa kwa ujumla.
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa