“Bila taarifa hakuna kazi uliyoifanya hivyo wataalam wa Afya mnao kwenda kushiriki zoezi hili la chanjo hakikisheni mnaweka taarifa sahihi ili tuweze kuwa na takwimu za walengwa waliopatiwa chanjo.” Hayo yamesemwa leo tarehe 20 February 2023 na Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa Ndg. Ally Rubeba wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha kuweka mikakati ya kuhakikisha kila mlengwa anapata chanjo stahiki katika wiki ya chanjo Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga.
Kuanzia tarehe 21 Februari hadi tarehe 28 Februari 2023 Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga inatarajia kutoa Chanjo za aina zote kwa watoto walio na umri chini ya miaka mitano kwa watoto ambao hawakumaliza chanjo, Chanjo ya kukinga Saratani ya Mlango wa kizazi (HPV) kwa wasichana kuanzia umri miaka 14 walioko shule za Msingi na Sekondari, pamoja na chanjo ya UVIKO 19 kwa wale ambao hawajachanja na ambao hawakumaliza chanjo ya pili.
Katika kikao kazi hiki cha Idara ya Afya, Wataalam wa Afya wamekubaliana kwa pamoja kuwa kuanzia sasa kila Kituo kihakikishe kinatunza vizuri taarifa na takwimu za walengwa kwa usahihi wakati wa zoezi hili la chanjo na taarifa zote zinaingizwa kwenye mfumo, kila Kituo kinatunza dozi za chanjo kulingana na Miongozo ya WHO ili chanjo hizi zisiharibike na kila kituo kinatoa dozi za chanjo kikamilifu kulingana na miongozo hasa kwa chanjo ambazo zina dozi zaidi ya moja kama vile chanjo ya Polio na HPV.
Mwakilishi wa WHO Ndg. Baraka Chaula amesema kuwa “tupende kuwapongeza Sekta ya Afya kwa kazi nzuri mnazofanya hasa kwa upande huu wa chanjo kwani kazi zenu zimekuwa na mafanikio makubwa kwa taifa hili kwa kipindi cha Miaka 23 Tanzania haijapata kisa cha Mgonjwa wa Polio”. Isipokuwa hatuweki taarifa zetu katika mifumo inayotakiwa hali iliyopelekea Tanzania kukosa Cheti cha “ Tanzania Huru Bila Polio” cheti ambacho kiilitakiwa kutolewa miaka nane iliyopita kulingana na Miongozo ya WHO
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa