Na. Mwanaidi Waziri
Mkuu wa wilaya ya Nkasi Said Mtanda ametangaza mkakati wa kuhakikisha watumishi wote ambao ni waajiriwa wa wilaya hiyo, ambao hawajapitia mafunzo ya JKT kuhakikisha wanapata mafunzo hayo ili kuweza kuimarisha ukakamavu na kuwajengea uzalendo wa kuitumikia nchi yao.
Agizo hilo limetolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama na Mkuu wa wilaya hiyo mwishoni mwa juma wakati akifunga mafunzo ya JKT kwa wahitimu wa kidato cha Sita kwenye Kikosi Cha 847 KJ kilichopo Milundikwa wilayani Nkasi
Alisema “tunaanza na wakuu wa Idara, watendaji wa kata, watendaji wa vijiji na hata waheshimiwa madiwani watahitaji mafunzo mwezi mmoja wakae hapa JKT na kufanya mafunzo ili wakiondoka hapa wawe wazarendo katika nchi yao”
Baadhi ya vijana wahitimu wa mafunzo hayo ya JKT kwa kipindi cha miezi mitatu wametaka vijana wenzao kutopata uoga iwapo watapata nafasi ya kujiunga na JKT, kwani wamebaini kuwa kuna mambo mengi ambayo yanazungumzwa mitaani yanayowavunja moyo vijana kuhusu mafunzo ya JKT kinyume na hali halisi iliyopo kwenye makambi hayo
Zaidi ya askari 500 wamehitimu mafunzo hayo ya JKT kwa mujibu wa sheria kwenye kambi ya Milundikwa wilayani Nkasi.
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa