Wasindikaji wa mazao mkoani Rukwa wametakiwa kusindika bidhaa zao kwa kufuata ushauri wa Wataalamu wa TBS ili kuweza kukidhi vigezo vinavyokubalika katika soko la ndani na nje ya nchi.
Ushauri huo umetolewa na Mkuu wa mkoa wa Rukwa Makongoro Nyerere wakati akifungua mafunzo ya siku mbili ya Wasindikaji na Wafanyabiahara wa mazao yaliyoandaliwa na Shirika la Viwango TBS Kanda ya Magharibi na kufanyika kwenye ukumbi wa halmashauri ya Manispaa Sumbawanga.
Mkuu huyo wa mkoa alisema ushirikiano wa Wasindikaji hao na Wakaguzi wa TBS utaongeza ubora wa bidhaa zinazozalishwa hivyo hakuna haja ya kundi hilo kuwakwepa au kuwachukia Wataalamu wa kada hiyo.
Alisema kundi hilo ni muhimu katika kuongeza pato la mkoa na Tfifa kwasababu wamekuwa wakilipa kodi hivyo liendelee kupewa mafunzo ya mara kwa mara ili kuweza kuzalisha kisasa kwa bidhaa zenye viwango.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Sumbawanga Nyakia Chirukile alisema ipo haja ya mkoa kwa kushirikiana na Wawekezaji kuweza kuanzisha kiwanda kikubwa cha usagaji na ufungashaji bidhaa za vyakula vya Wanga na kuuza nchi za nje ambako bado kuna mahitaji makubwa ya soko , lakini pia itachangia kuibua ajira kwa vijana.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga Thadeo Maganga alishauri Wasindikaji hao kuhakikisha wanaweka viini lishe kwenye unga wanaosaga ili kuweza kuongeza virutubisho kwa walaji.
Naye Meneja wa Mafunzo wa TBS Kanda ya Magharibi Soud Mwansala alisema utoaji wa mafunzo kwa Wasindikikaji hao ni utaratibu endelevu kwao ili Taifa liweze kusindika bidhaa bora zinazokidhi vigezo vya masoko.
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa