By Kisika S- Kitengo cha Mawasiliano SMC
Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga imetakiwa kuendesha zoezi la kuwaondoa watoto wa miaani na kuwakabidhi kwa wazazi au walezi wao.
Agizo la Mkuu wa wilaya ya Sumbawanga Nyakia Ally Chirukile katika kikao cha Baraza la Madiwani wa halmashauri hiyo.
“Naamini mtaa hauwezi kuzaa mtoto na hawa waliopo wana wazazi kama sio walezi wao, hivyo tunapaswa kuhakikisha wanaondoka mitaani kwasababu kuendelea kuwalea tunajitafutia makubwa zaidi siku za usoni” alisema Nyakia
Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Manispaa ya Sumbwanga Justine Malisawa alisema haingii akilini kuona mkoa wa Rukwa ambao ni mmoja ya mikoa Sita inayoongoza kwa uzalishaji wa chakula nchini unakuwa na watoto ombaomba.
Afisa Maendeleo ya jamii Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga Frank Mateni alisema mji wa Sumbwanga unakadiriwa kuwa na watoto wa mitaani wapatao Miambili iatano hadi Miatano.
Mateni alisema wamekuwa wakiendesha zoezi la kuwakamata watoto hao na kuwapeleka kwenye ofisi za kata zinazowakutanisha na wazazi au walezi wao na wapo ambao wanasadhibiwa kwa kutozwa faini ya Sh.50,000/- lakini baada ya muda wanarejea tena mitaani.
“… Wengi wao wanafanya kazi ya kuombaomba, kufanya vibarua na kujipatia fedha ndogo, lakini kundi kubwa limeonekana kutumwa na wazazi wao kuomba mitaani.”alisema Mateni.
Alisema halmashauri hiyo iko kwenye mipango ya kuitisha mkutano na wadau wa mtoto ili kujadili namna ya kuliondoa kundi hilo mitaani.
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa