Wananchi wa Manispaa ya Sumbawanga wameshauri kujenga tabia ya kupenda kuchangia masuala ya kielimu badala ya kuendekeza kuchangia sherehe na mambo mengine ya kistarehe.
Wito huo umetolewa na Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Mh.Justine Malisawa wakati akifungua warsha ta wadau wa elimu katika halmashauri hiyo katika ukumbi wa Manispaa, kwaajili ya kutathimini maendeleo ya elimu katika shule za Msingi na sekondari katika Manispaa hiyo.
Mstahiki Meya huyo alisema ipo tabia ya wananchi wa Manispaa hiyo na mkoa wa Rukwa kwa ujumla kurudi nyuma pale inapotokea wanatakiwa kuchangia kutatua changamoto mbalimbali za kielimu katika shuke za Msingi na Sekondari zilizopo kwenye maeneo yao.
“Laiti kama ningelitangaza kuwa naomba michango yenu kwaajili ya sherehe ya Kipaimara kwa mwanangu nadhani huu ukumbi ungelijaa watu na michango ingelikuwa mingi sana, lakini kama nitatangaza kuomba michango ya ujenzi wa choo katika shule ya Msingi Kihwelu hapa utaona kila mtu anabidiika na simu yake kama anazungumza na kutoka nje akikwepa kuchangia mchango huo wa kielimu”.alisema Mh. Mwanisawa
Hatahivyo Mstahiki Meya huyo aliwataka wananchi wa Manispaa hiyo kubadili mtazamo wao na kuongeza kuwa katika Ulimwengu wa sasa kila sehemu suala la elim u limepewa kipaumbele.
Aidha katika hatua nyingine Mestahiki Meya huyo wa Manispaa ya Sumbawanga amewataka viongozi na Watendaji mbalimbali wa Idara katika Manispaa hiyo kujenga utamaduni wa kutoa motisha kwa watumishi wake hususan wale wa Idara ya elimu kwa walimu wakuu au wakuu wa shule waliofanya vema katika ufaulu wa wanafunzi wao katika matokeo Darasa la Saba, Kidato cha pili na kidato cha Nne na Sita.
Katika matokeo ya Darasa la Saba mwaka 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Sum bawanga ilishiuka nafasi ya 33 katika halmashauri zote hapa nchini.
.
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa