Manispaa ya Sumbawanga unakusudia kuendesha kampeni ya kuwabaini wakazi wote wa Manispaa hiyo wanaoishi kata za mjini halisi ambao wamekaidi kutii sheria ndogo ya kutolima mazao yenye urefu wa zaidi ya mita moja kwenye maeneo yao.
Agizo la Mstahiki Meya wa Manispaa ya Sumbawanga Justine Malisawa kwenye kikao cha Baraza la Madiwani linasema kuwa siku nyingi tangia katazo la kutolima mazao hayo yakiwapo mahindiambayo baadhi ya wananchi wamekuwa wakilima na kuwa chanzo cha uchafu mjini.
“ Sheria iko wazi juu ya aina ya mazao yaya kulimwa mjini lakini kuna watu kwa makusudi wanaamua kukaidi, sasa tutawasaka na kuwachukulia hatua za kisheria ili wajutie ukaidi huo.”
Meya Malisawa alisema safari hii hakuna hatua ya kufyekewa mazao ambayo itachukuliwa na badala yake wahusika wataadhibiwa kwa mtindo huo na kuongeza kuwa hata Watumishi wa serikali wenye dhamana ya kusimamia masuala ya usafi kwenye kata nao wataadhibiwa kwa kushindwa kutimiza wajibu wao wa kuhakikisha mazao hayo hayalimwi mjini.
Alisema ulimaji wa mahindi mjini umekuwa ukichangia watu wengi kuzoa taka na kuzitupa kwenye mashamba hayo hivyo kuwa kichocheo cha ugonjwa wa KIpindupindu ambao umeripotiwa kwenye mikoa jirani hadi sasa.
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa