Ameandika Kisika.
Wafanyabiashara na Wajasiriamali mkoani Rukwa wameaswa kuzingatia sheria za nchi na miiko ya biashara zao ili waweze kukabiliana na changamoto za mtikisiko wa kiuchumi unaoendelea kote Dunia hivi sasa.
Akizungumza wakati akiwasilisha mada ya elimu ya ujasiriamali Mwezeshaji kutoka Chuo cha Sayansi na Teknolojia MUST tawi la Mbeya Dk.Lulu Luflenge amesema Duniani inapitia kwenye mabadiliko makubwa ya kiuchumi katika kipindi hiki cha mlipuko wa ugionjo wa Uviko-19 na vita vya Ukraine na Urusi hivyo wanapaswa kuwa makini katika uendeshaji wa biashara zao.
Katika mkutano wa Wafanyabiashara wanaohudumiwa chini ya Benki ya NMB mkoani Rukwa, Dk.Lulu alisema pamoja na kuwapo kwa changamoto hizo za kiuchumi ni vizuri Wafanyabiashara wafuate maagizo yanayotolewa na halmashauri zao na Mamlaka ya Mapato (TRA) ili kuweza kuepuka ukiukaji wa sheria ambao unapelekea baadhi yao kujikuta wakipigwa faini.
“Tunasema uchumi umebana lakini unakiuka sheria, unapopigwa faini inaathiri biashara yako kwasababu hizo fedha unazotoa faini ungezitumia kwaajili ya kuongeza mtaji wa biashara hiyo”. Alisema Dk.Lulu
Hatahivyo aliwashauri wafanyabiashara hao kujenga utaratibu wa kutangaza biashara zao badala ya kukaa kimya ukijifaraji kuwa unafahamika, jambo ambalo halijengi uimara wa biashara zao.
Pia aliwataka kuzidi kujifunza elimu ya biashara ikiwa na pamoja kuwa na kauli nzuri zenye kuvutia wateja sanjari na kutumia sehemu ya faida kwaajili ya kuburudika katika maeneo mbalimbali hususan yale ya kitalii angalau mara moja kwa mwaka kuliko kujifungia eneo moja siku zote.
Kwa upande wake Meneja wa NMB Kanda za Nyanda za Juu Kusini Straton Chilongola alisema mkakati wa Benki hiyo ni kuhakikisha inatoa huduma bora za kifedha kwa wateja wake sanjari na kuwapa elimu ya biashara.
Baadhi ya Wafanyabiashara wameishukuru Benki hiyo kuendeleza utaratibu wa kuwakutanisha kupitia Klabu ya Wafanyabiashara ambapo wanapata fursa ya kujadili pamoja changamoto zao.
Klabu ya wafanyabiashara ya NMB mkoani Rukwa inajumuisha makundi yote ya wafanyabiashara mkoani humo ambao ambao wamekuwa wakifanya biashara ndogo na kubwa.
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa