Ofisi ya Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga imewatahadharisha wakazi wa Manispaa hiyo kutotumia simu za kisasa kwaajili ya vipimo vya Afya zao.
Tahadhari hiyo imetolewa kufuatia kuzagaa kwa taarifa zinazoenea mjini hapo kuwa wapo watumiaji wengi wa simu za mkononi za kisasa zenye uwezo wa Android ambao wamekuwa wakipakua baadhi ya mifumo wanayoitumia kupima Virusi vya Ukimwi, Mimba, Presha na hata makundi ya damu zao.
Mganga Mkuu wa Manispaa ya Sumbawanga Dkt. Archie Hellar alisema kuwa uongozi wa halmashauri hiyo umekutana na kutaka tahadhari itolewa kwa wananchi kutokana na mkanganyiko huo.
Dkt. Hellar alisema hakuna taarifa za kitaalam zilizotolewa na Wizara ya Afya ambazo zinahalalisha kuwa simu za Android zinauwezo wa kupima HIV,mimba , BP na makundi ya damu kwa mtu yeyote, hivyo kuwataka wananchi kuzipuuza taarifa hizo.
Alisema kuendelea kutumiwa kwa teknolojia hiyo pasipo kuthibitishwa na Wataalam wa Afya kunaweza kuleta migongano katika jamii na ndio maana uongozi wa Manispaa hiyo umeamua kuwatahadharisha wananchi wake.
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa