Imeelezwa kuwa vikundi vya Huduma ndogo za fedha katika Manispaa ya Sumbawanga vimekuwa vikikosa sifa ya kukopesheka kutokana na kutumia Wahamasishaji wasio na sifa katika shughuli zao za kila siku.
Akizungumza na vikundi hivyo Mratibu wa Huduma ndogo za Kifedha katika Manispaa ya Sumbawanga Mahamoud Mohamed amesema vikundi hivyo vimekuwa vikikosa mikopo hiyo licha ya kuwa ni haki yao kupewa mikopo hiyo kulingana na sheria, kanuni taratibu zilizowekwa na serikali na taasisi za kifedha.
Katika kuondoa dosari hiyo ofisi ya Mratibu huyo wa Huduma ndogo za kifedha kwa kushirikiana na Wataalamu wengine wametoa mafunzo ya kwa vikundi hivyo kwa lengo la kuwajengea uwezo kuhusu mfumo wa usajili wa Benki Kuu na watoa huduma ndogo za kifedha.
Mahamoud alisema kuwa Wahamasishaji wasiosajiliwa wamekuwa wakitumia vikundi vyao kama fursa ya kujinufaisha wao, huku baadhi ya vikundi vikidhulumiwa kutokana na kutozwa gharama mbalimbali za kuandaaji katiba, fomu za mikopo.
Katika kuepukana na kadhia hiyo vikundi hivyo vimeshauriwa kuwa na usajili wa Benki ili kuweza kufanya biashara zao kihalali na kupunguza migogoro kwenye vikundi hivyo.
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa