Inaandikwa na Sammy Kisika.
Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga inakusudia kuvikisha mahakamani vikundi 58 vinavyodaiwa zaidi ya Shilingi Milioni 100 vilivyopatiwa mikopo ya asilimia 10 ya Wajasiriamali na halmashauri hiyo kwa kipindi cha miaka miwili pasipo kuirejesha jambo ambalo linakiuka malengo ya mikopo hiyo.
Akizungumzia mikopo Afisa Vijana na Mikopo wa halmashauri hiyo Mahamoud Mohamed alisema mikopo hiyo ni ile ambayo ilitolewa kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2018 hadi 2020 kwa vikundi vya vijana, wanawake na walemavu.
Mahamoud alisema kuwa tayari wamewasiliana na viongozi wa vikundi hivyo kuwakumbusha kuhusu kurejesha mikopo hiyo lakini baadhi yao wameendelea kupuuzia.
Afisa huyo wa vijana alisema ni muhimu kwa vikundi hivyo kutambua umuhimu wa kurejesha mikopo hiyo ili watu wengime nao pia wapate kukopa.
“Hii mikopo sio hisani, hivyo wanavikundi wanatakiwa kulitambua hilo, vinginevyo watachukua hatua hizo ili mahakama ifanye kazi yake”.alisema Mahamoud
Katika mwaka wa fedha wa 2018/19 hadi 2019/220 halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga ilikopesha zaidi ya Shilingi Milioni 400 ikiwa ni makusanyo ya ndani na kutoa asilimia 10 kwa makundi hayo.
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa