• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe za wafanyakazi |
SUMBAWANGA MUNICIPAL COUNCIL
SUMBAWANGA MUNICIPAL COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Manispaa
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Masuala ya Lishe
      • Idara ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Uratibu na Mipango
      • Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasimali watu
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
        • Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Utunzaji wa Mazingira
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati na majukumu yake
      • Fedha na Utawala
      • Uchumi, Elimu & Afya
      • Mipango miji & Mazingira
    • Ratiba za Vikao
      • For Councilors
      • For Hon. Mayor
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Fomu
    • Taratibu
    • Huduma za Kisheria
    • Fedha
  • Kituo cha Habari
    • Albamu ya Picha
    • Video
    • Taarifa Kwa Umma
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio
    • Makala
    • Michezo & Burudani

Vijana, wanawake na walemavu wala neema Manispaa ya Sumbawanga

Ilibandikwa: November 9th, 2018

Halmashauri ya manispaa ya Sumbawanga imetoa shilingi milioni 70.5 kwa vikundi 21 vya vijana, wanawake na walemavu ikiwa ni utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ya Mwaka 2004 yenye adhima ya kuwainua wananchi kiuchumi ili kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Manispaa ya Sumbawanga imedhamiria kutekeleza maelekezo ya serikali kwa kutenga asilimia 10 ya mapato ya ndani na kuwezesha vikundi hivyo ambapo tangu mwaka wa fedha 2018/2019 uanze mwezi Julai hadi mwezi Novemba Halmashauri tayari imeshakusanya Shilingi bilioni 1.1 ambayo ni nusu ya makusanyo ya malengo waliyojiwekea kwa mwaka huu.

Fedha hizo zilitolewa katika hafla fupi ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo aliyekabidhi hundi kwa vikundi hivyo na kuhudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dkt. Khalfan Haule, Meya wa Manispaa ya Sumbawanga Mh. Justin Malisawa na viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa na vikundi husika.

Akisoma taarifa ya kukabidhi fedha hizo kwa vikundi Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga Jacob Mtalitinya alisisitiza kuwa Ili dhamira ya Serikali ya kufikia uchumi wa kati na Tanzania yenye Viwanda itimie shughuli utoaji wa mikopo lazima iwe endelevu na kuwa halmashauri imejiimarisha katika kukusanya mapato yake ya ndani ili kuleta matunda kwa kutoa mikopo.

“Vikundi hivi  vinajishughulisha na Usindikaji mafuta, chakula,vinywaji, Useremala, Utengenezaji wa Chaki na ushonaji, ufumaji na utengenezaji wa Mabatiki na Ufugaji wa kuku na ngombe wa maziwa. Pia Halmashauri inatarajia kutoka kiasi cha mkopo kilichobakia kwa mwezi Januari, 2019 kitakachokuwa kimekusanywa kutokana na makusanyo ya ndani.” Alisema.

Aliongeza kuwa ili kuona vikundi hivyo vinakuwa kiuchumi maafisa maendeleo ya jamii  ngazi ya kata na halmashauri kuhakikisha wanakuwa na orodha ya vikundi vilivyokopeshwa, kwaajili kufuatilia shughuli za vikundi na kuwajengea uwezo pamoja na kubaini mwendo wa urejeshaji wa mikopo kwa vikundi  na kufanya ufuatiliaji wa marejesho ya mikopo.

KWa upande wake Mh. Wangabo aliipongeza Manispaa ya Sumbawanga na kwaagiza wakurugenzi wote wa halmashauri zizlizopo Mkoa wa Rukwa kuhakikisha wanatekeleza agizo hilo ili kuweza kukuza kipato cha mwananchi wa Mkoa kwa kuwawezesha kiuchumi na hatimae kuongeza ajira pamoja na kukuza uchumi wa viwanda.

Pi aliwapongeza wale waliofanikiwa kupata mikopo hiyo na kuwasihi waweze kurudisha kwa wakati ili na wengine wapate fursa ya kukopeshwa na kujikwamua na kuwaonya kutotumia fedha hizo kwa matumizi ambayo yako tofauti na walichoombea.

“Serikali haitafurahishwa kuona fedha zilizokopwa zinatumika kwa malengo ambayo hayakukusudiwa kama vile anasa, aidha, nitoe wito kwa Wakurugenzi wa Halmashauri zote ndani ya Mkoa wetu kupitia hafla hii, kuweka mipango na mikakati ya kuhakikisha wananchi wanawezeshwa kiuchumi ikiwa ni pamoja na kuwaunganisha na wadau mbalimbali wa maendeleo  ndani na nje ya Mkoa kwa kadiri itakavyowezekana.”Alisisitiza.

Kuanzia mwaka 2013/2014 hadi 2017/2018 fedha zilizopaswa kuchangiwa na Halmashauri yetu kama asilimia 10 ya mapato ya ndani ni shilingi 684,055,823. Hata hivyo hadi kufikia Juni 2018 jumla ya shilingi 50,000,000 zilitolewa kwa vikundi 43 sawa na asilimia 7.3 ya lengo. kiasi cha shilingi 634,055,823 hakikutolewa kutokana na mwenendo wa makusanyo.

Matangazo

  • TANGAZO LA CHANJO KWA WATOTO CHINI YA UMRI WA MIAKA MITANO April 26, 2023
  • RATIBA YA MTIHANI WA DARASA LA SABA 2023 March 11, 2023
  • RATIBA YA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA 2023 March 11, 2023
  • TANGAZO LA ZABUNI YA KAZI ZA UBORESHAJI WA BARABARA KATIKA MANISPAA YA SUMBAWANGA March 01, 2023
  • Angalia zote

Habari za Karibuni

  • SHIRIKIANENI NA SERIKALI KULETA MAENDELEO RUKWA-RC MAKONGORO

    March 16, 2025
  • MD PENDO MANGALI-MSIWE MADALALI WA VIWANJA, CHAPENI KAZI

    November 28, 2024
  • KUITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA MANISPAA SUMBAWANGA

    October 01, 2024
  • EDWINE MISASI NAIBU MEYA MPYA MANISPAA YA SUMBAWANGA

    August 27, 2024
  • Angalia zote

Video

MANISPAA YA SUMBAWANGA KUTAFUTA MZABUNI WA KUZOA TAKA
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • History
  • Councilors
  • Photo Gallery

Viunganishi vinavyofanana

  • Public Servant portal
  • Download your Salaryslip here
  • Looking for a job in Public Sector?
  • Get everything from the government
  • Rukwa
  • TAMISEMI

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya wageni

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Sumbawanga Municipal Council

    Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga

    Simu ya Mezani: +255252802163

    Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255

    Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Uhuru binafsi
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa