Anaandika Sammy Kisika.
Mahakama Kuu ya Tanzania imeshauriwa kuendeleza utaratibu mpya wa kuaga Majaji wastaafu wa Mahakama hiyo, ambao wamelitumikia Taifa kwa uadilifu huku wakiacha alama katika tasnia ya sheria ambazo zinaweza kutumika kama nyaraka kwaajili ya kufundishia kizazi kijacho katika vyuo vya sheria.
Ushauri huo umetolewa na Mwakilishi wa Mkuu wa mkoa wa Rukwa ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Sumbawanga Sebastian Waryuba, mara baada ya kwisha kwa Shauri dogo la Kitaaluma Namba 1 la mwaka 2022, shauri la kuenzi kazi za Kitaaluma na kumwaga Mh. Jaji David Mrango aliyekuwa Jaji wa Mahakamu Kuu Kanda ya Sumbawanga, lililosikilizwa na Jaji Kiongozi Mustapher Siyani.
Shauri hilo la aina yake katika Mahakama hii lilisomwa mahakamani hapo na Msajili wa mahakama nchini Mh.Shamira Salawati ambaye alilitaja kuwa ni lakitaaluma kwa lengo la kuenzi utumishi wa Jaji Mrango aliyestaafu akiwa Jaji tangia mwaka 2014.
Unaweza fikiri kuwa ni kesi rasmi lakini kumbe ni shauri la kuigizwa ukiwa ni utaratibu wa Mahakamu Kuu kuwaaga Majaji waliotumikia kada hiyo na kustaafu kwa taratibu za kiserikali baada ya umri wao wa utumishi kukoma.
Mkuu wa wilaya ya Sumbawanga Sebastian Waryuba aliuopongeza utaratibu huo wa Mahalama Kuu wa kuwaaga Majaji wake wanaoustaafu kwasababu unaleta chachu kwa watumishi wengine wa kada hiyo ambao nao wanataraji kustaafu kwa heshima baada ya kuitumikia serikali kwa muda mrefu.
Mwanasheria Mwandamizi wa serikali Simon Pares yeye alisema Jaji Mstaafu Mrango atakumbukwa kwa tabia yake kupinga vitendo vya rushwa ambao alikuwa hajali uwezo wa mtu katika kutenda haki.
Naye Wakili Msomi Bartazary Chambi yeye alimsifu Jaji huyo mstaafu kwa kupenda kuzingatia muda katika utendaji wake wa kazi na alikuwa mnyenyekevu kwa kila mtu licha ya kuwa alikuwa na nafasi kubwa katika kada hiyo ya sheria.
Shauri hilo la aina yake ambalo linatoa funzo la uadili katika utumishi wa umma lilihitimishwa na Jaji Kiongozi Mh.Mustapher Siyani akiwa na Majaji wengine Sita ikiwa ni ishara ya kubariki kustaafu kwa Jaji Mrango
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa