Serikali inatarajia kujenga hospitali mpya ya rufaa ya mkoa wa Rukwa ili kupunguza msongomano wa wagonjwa katika hospitali ya sasa ya mkoa.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Zelothe Steven Zelote, alisema hospitali ya sasa ya mkoa, inaelemewa na idadi kubwa ya wagonjwa wanaofi ka kutibiwa.
Mh. Zelothe alieleza tayari eneo la ardhi kwa ajili ya ujenzi wa hospitali hiyo mpya, limepatikana na fi dia imeshatolewa kwa wananchi ili kupisha ujenzi wake.
Alisema hayo alipozindua huduma ya madaktari bingwa chini ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), walioletwa mkoani Rukwa kutoa huduma mbalimbali kwa wagonjwa kuanzia Julai 3 hadi 8, mwaka huu .
Madaktari bingwa saba watatoa matibabu ya kibingwa kwa magonjwa mbalimbali yakiwemo ya watoto, wanawake na mfumo wa uzazi, mfumo wa mkojo, mfumo wa pua , koo masikio na magonjwa ya moyo na ya ndani.
Hafla hiyo ilifanyika viwanja vya Hospitali ya mkoa wa Rukwa mjiniSumbawanga.
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa