Serikali imetenga zaidi ya Shilingi Bilioni 10.7 kwaajili ya ujenzi wa chuo cha Ufundi Stadi VETA ambacho kinatarajiwa kujengwa katika eneo la Muva kata ya Sumbawanga katika Halmashauri Manispaa ya Sumbawanga.
Akizungumza katika hafla fupi ya makabidhiano ya kati ya serikali na mkandarasi atakayejenga chuo hicho Kaimu Mkuu wa mkoa wa Rukwa ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Sumbawanga Dkt.Halfan Haule alisema ujenzi wa chuo hicho unaondoa kiu ya muda mrefu ya wananchi wa mkoa wa Rukwa ambao walikuwa wakihitaji kupata chuo cha aina hiyo.
Dkt.Haule alisema kuwa kupatikana chuo hicho ni ukombozi kwa wakazi wa mkoa wa Rukwa hususan vijana ambao watajifunza mambo mengi ikiwa ni pamoja na ujasiriamali na usindikaji wa mazao yao.
Aidha alisema jumla ya majengo tisa likiwapo jengo la utawala yatajengwa huku akitoa wito kwa wakazi wa eneo hilo kuchangamkia fursa hiyo kupata ajira za muda mfupi kwa kufanya kazi za vibarua wakati wa ujenzi huo.
Hatahivyo aliwataka wazazi mkoani Rukwa kutumia fursa hiyo kwa kuwahimiza vijana wao kusoma kwa bidii ili wapate nafasi ya kujiunga na chuo hicho, huku wakitumia mwanya huo kama njia mbadala ya kuendelea na masomo ya elimu ya juu katika masuala ya teknolojia.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa VETA Hildegareis Bitegera alisema chuo hicho kitajengwa na kampuni ya Tendar International Co.Ltd na unataraji kuchukua muda wa muda wa miezi 12 hadi kukamilika kwake.
Alisema jumla ya wanachuo 1500 wanatarajiwa kudahiriwa katika kipindi cha mwaka mmoja, wakiwapo wanachuo wa 600 watakaokuwa wakisoma kozi za muda mrefu na wengine watasoma kozi za muda mfupi.
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa