Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga Jacob Mtalitinya amesema wanatarajia kukakamilisha kazi zote za madarasa ifikapo Desemba 20, kisha kuyakabidhi kwa Mkuu wa wilaya ya Sumbawanga Sebastian Waryuba.
Akizungumza na Timu ya Wataalamu wa Manispaa hiyo mara baada ya kukagua maendeleo ya miradi ya ujezni wa madarasa hayo ya Uviko-19, Mtalitinya alisema kuwa sehemu nyingi walizotembelea ujenzi umefika zaidi ya asilimia 90 huku mengine yakiwa yamekamilika kabisa.
Mkurugenzi huyo alisema kuwa tayari wameytoa maelekezo kwa shule ambazo hazikamilisha, kufanya kazi usiku na mchana na kukamilisha kabla ya Desemaba 19, ili waweze ,kukabidhi ifika Desemba 20.
"Mikakati yetu ya kusimamia ujenzi wa madarasa imekwenda vizuri na tunaamini kuwa itakuwa ni miradi bora kuliko yote katika mkoa wetu, kwasababu tumezingatia vigezo vyote vya muhimu na usimamizi ulikuwa wa karibu zaidi.
"Tunaishukuru serikali kwa kutupatia fedha hizo ambazo zimepunguza upunghufu wa madarasa ambayo yalikuwa yakihitajika kujengwa kwaajili ya kupokea wanafunzi wa Kidato cha Kwanza 2022".alisema Mtalitinya.
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa