Mbunge wa Jimbo la Sumbawanga Mjini Aesh Hilaly amewashauri Wataalamu wa Manispaa na viongozi wa serikali mkoani Rukwa kufanya maamuzi magumu ili kuweza kuinusuru stendi ya mabasi ya Katumba-Azimio iweze kufanya kazi muda wote.`
Mbunge huyo alitoa wito huo kwenye kikao cha Baraza la Madiwani la kumaliza mwaka ambapo alisema kuwa anasikitishwa na hali ilivyo hivi sasa kwenye stendi hiyo ambayo imejengwa kwa mabilioni ya fedha lakini haitumiki ipaswavyo baada ya kufunguliwa na kufanya kazi kwa muda mfupi na shughuli nyingi kuhamishiwa stendi ya zamani ya Sokomatola.
Alisema mashinikizo ya watu ambao wana maslahi kisiasa yanafanya kudorora kwa stendi ya Katumba jambo ambalo sio sahihi kwasasa kutofanya kazi kwa kituo hicho cha mabasi na kuongeza kuwa ni matumizi mabaya ya fedha za serikali zilizotumika kujenga stendi hiyo ya kisasa.
’’Kinachosemwa kuwa ni umbali wa stendi iliko sio sahihi, ebu tujifunze kwa wenzetu wa Dodoma, Iringa, Dar es salaam, stendi zao ziko nje ya mji lakini zinatumika, hii leo sisi tunasema kule ni mbali, kwanini tunakubali hayo maneno ya baadhi ya Wanasiasa”.alisema
Stendi ya mabasi ya Katumba Azimio imejengwa gharama ya takribani Bilioni 9.
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa