Wamiliki na wauzaji wa maduka ya madawa muhimu kwenye mikoa ya Nyanda za Juu Kusini wametakiwa kuzingatia miongozo inayotolewa na serikali juu ya matumizi sahihi ya dawa zinazouzwa kwa wateja wao kwa kuuza dawa ambazo zimekwisha muda wake jambo linalochangia wagonjwa kupata madhara kiafya na wengine kupoteza maisha.
Wito huo umetolewa na Kaimu Meneja wa TMDA Nyanda za Juu Kusini, Anitha Mshigati wakati mafunzo ya matumizi sahihi ya madawa na vifaa tiba yaliyofanyika mkoni Rukwa ili kuwajengea uwezo wauzaji na wamililiki wa maduka hayo kuweza kutoa huduma sahihi zinazoendana na wakati kwa kujali afya za wateja wao.
Mshigati amesema TMDA kwa kushirikiana na vyombo vingine vya serikali katika mwaka wa fedha wa 2020/21 wamefanya ukaguzi kwenye maduka mbalimbali ya madawa na kukamata zaidi ya tani tatu za dawa na vifaa tiba vyenye thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni 30 ambavyo vilikuwa vikiuzwa ihali muda wake wa matumizi ukiwa umekwisha au havikusajili au kukosa sifa ya matumizi hivyo waliamua kuviteketeza.
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa