Shirika la Tanesco Mkoani Rukwa linatarajia kuanza zoezi la kuchukua taarifa za kijiografia za Miundombinu ya Shirika, Rasimali na Wateja wao mapema baada ya zoezi hili kukamilika Mkoani Songwe.
Wataalam kutoka Shirika la Tanesco watapita nyumba kwa nyumba kwa ajili ya kupata taarifa za miundombinu ya Shirika na kupata taarifa sahihi za wateja wao. Zoezi hili lina maufaa makubwa sana katika kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi na Mpango na Malengo ya Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Zoezi hili litasaidia kuongeza ufanisi katika kutoa huduma kwa wateja ambapo mteja akitoa taarifa ya changamoto katika eneo lake atapatiwa huduma kwa haraka na kwa wakati. Pia zoezi hili litasaidia kuboresha usimamizi wa rasimali za Shirika.
Wakati wa zoezi hili Shirika la Tanesco linaomba ushirikiano mkubwa kutoka kwa wananchi kwa kuwapatia wataalam wa Shirika namaba za simu za Mmiliki wa nyumba nan amba ya mita kwani zoezi hili linafanyika bure pasipokuwa na malipo yoyote.
Hayo yamesemwa leo tarehe 23 Februari 2022 na timu kutoka Shirika la Tanesco mkoa wa Rukwa ilipofika katika ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga ilipofika kutambulisha umuhimu wa zoezi hili kwa wananchi na taifa kwa ujumla
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa