Wananchi mkoani Rukwa wametahadharishwa kuwa makini dhidi ya Ugonjwa wa Ebola ulioripotiwa kuibuka kwenye nchi jirani ya Congo DRC.
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Zelote Steven Zelote ametoa tahadhari hiyo wakati akizungumza na Madiwani wa halmashauri zote nne za mkoa wa Rukwa kwenye ukumbi wa RDC siku chache baada ya nchi ya Congo DRC kukumbwa na ugonjwa huo huku mkoa wa Rukwa ukiwa ni mmoja ya mikoa inayopakana nan chi hiyo ihali kukiwa na mwaingiliano mkubwa wa raia wanchi hiyo na Tanzania, hususa katika maeneo ya mwambao mwa Ziwa Tanganyika.
Kwa upande wake Kaimu Mganga Mkuu wa mkoa wa Rukwa Dkt. Emmanuel Mtika amesema licha kuwa hadi hivi sasa hakuna tukio lililoripotiwa kuwepo kwa ugonjwa huo hapa nchini lakini tahadhari inatakiwa kuchuliwa ili Taifa lisiweze kukubwa na madhara ya ugonjwa huo ambao matibabu yake yanagharama kubwa mno.
“Kwanza tukumbuke bado ugonjwa wenyewe hauna kinga wala tiba na kinachofanyika ni kutiba zile homa zinazoonekana kwa mgonjwa huyo na gharama ya kumtibu mgonjwa mmoja ni sawa na bajeti ya mwaka mzima kwa halmsahauri moja hapa nchini.” Alisema Dkt. Mtika.
Alizitaja baadhi ya dalili za ugonjwa huo kuwa ni pamoja namgonjwa kupata, homa kali, kutapika mfululizo, maumivu ya kichwa, kutokwa damu katika kila sehemu ya tundu la mwili wa binadamu nk.
NJIA ZA KUEPUKA UGONJWA HUO.
MIKAKATI YA MKOA KUKABILIANA NA UGONJWA USIWEZE KUINGIA NCHINI
NB. Wananchi wanashauri kutokuwa na hofu kwani hadi hivi sasa hakuna mtu yeyote aliyebainika kuwa na ugonjwa huo japokuwa tahadhali zinahitajika kuchukuliwa kwa kiasi kikubwa.
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa