Taasisi za serikali zinazopata huduma za matengenezo ya magari yao kwa Wakala wa serikali wa TEMESA mkoani Rukwa zimetakiwa kulipa madeni wanayodaiwa kwa muda mrefu ili kuwezesha Wakala huyo kujiendesha na kupata ufanisi kwenye utoaji wa huduma bora.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa mkoa wa Rukwa Charles Makongoro Nyerere katika mkutano wa TEMESA na Wadau wanaopata huduma na wale wanaoshirikiana na Wakala huo kwa lengo la kufanya tathimini na kutatua changamoto zao.
Mkuu wa mkoa huyo alibainisha kuwa katika mkoa wa Rukwa taasisi za kiserikali zinadaiwa zaidi ya Shilingi Milioni 500 kutokana gharama za magari yao wanayoyatengeneza TEMESA na kuyachukua pasipo kulipa kwa ahadi kuwa fedha italipwa baadaye.
“ Kwa hali hiyo usitaraji kuwa TEMESA ifanye vizuri licha ya kwamba nao wamekuwa wakilaumiwa katika huduma nyingi wazitoazo ikiwapo gharama kubwa za matengenezo, utaalamu usioridhisha, kuchelewesha matengenezo na mambo mengine”. Alisema Makongoro.
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa