Kazi ya ujenzi wa vyumba 49 vya madarasa katika Manispaa ya Sumbawanga inaendelea kwa kasi na mengi yakielekea ukingoni tayari kwaajili ya kuchukua wanafunzi wa Kidato cha mwakwa 2022.
Pamoja na changamoto za wali za kazi hii ikiwapo uhaba wa saruji na kupanda wa bidhaa za ujenzi Wataalamu wa Manispaa ya Sumbawanga, Wakuu wa shule na Kamati za ujenzi zinashirikiana kwa karibu kuhakikisha kazi hiyo hailali.
Hivi karibuni Naibu Waziri wa TAMISEMI David Silinde alifanya ziara katika Manispaa ya Sumbawanga na kushuhudia baadhi ya maeneo kazi ikiendelea na mwisho wa siku hakuficha hisia zake na kutamka kuwa anafurahishwa namna kazi inavyoendelea lakini pia ubora wa madarasa hayo yanayojengwa.
“Manispaa ya Sumbawanga ni moja ya eneo la kuigwa, nawapongezeni nyote akiwapo Mkurugenzi wa halmashauri Jacob Mtalitinya, Mbunge, Madiwani, Wakuu wa Sghule na wengine wote, kazi ni nzuri. Endeleeni hivyo hivyo” alisema Silinde.
Aidha Naibu Waziri huyo alizitaka halmashauri zingine mkoani Rukwa kuiga mfano wa Manispaa ya Sumbawanga kwa namna walivyojipanga kusimamia ujenzi huo wa vyumba vya madarasa.
Alisema fedha hizo zilizotolewa na Rais Samia Suluhu zinapaswa kuacha alama chanya kwenye sekta ya elimu, hivyo madarasa hayo lazima yawe ya mfano.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Sumbawanga Aesh Hilaly yeye aliomba serikali kuongeza fedha zingine ili ziweze kujenga vyoo vya kisasa kwa wanafunzi hao ambao shule nyingi za sekondari hazina vyoo licha wingi wa wanafunzi waliopo.
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa