Imebainishwa takribabi watoto Laki Tano wenye umri wa chini ya miaka Mitano hawakupata chanjo ya ugonjwa wa Polio katika kipindi cha mwaka 2020 hadi 2022 kutokana na sababu nbalimbali ikiwapo wazazi kutowapeleka kwenye vituo vya afya kwenda kupata chanjo hizo kwenye maeneo mbalimbali nchini.
Akisoma hotuba kwa niaba ya Waziri wa Afya Ummy Mwalimu, Mkuu wa mkoa wa Rukwa Charles Makongoro Nyerere katika uzinduzi wa zoezi la Chanjo ya Polio lililofanyika kwenye viwanja vya Ndua mjini Sumbawanga alisema kundi hilo linakwenda sanjari na watoto zaidi ya Milioni moja walioshindwa kupata chanjo ya kwanza ya Penta, hali ambayo ni kinyume na miongozo ya Wizara ya Afya katika kuwakinga watoto walio chini ya umri wa miaka mitano.
Aidha Waziri Ummy aliwataka Wakuu wa wilaya na Wakurugenzi wa halmashauri kwenye mikoa ambayo zoezi la chanjo ya Polio linatolewa kwa watoto walio chini ya umri wa miaka minane kuhakikisha wanasimamia zoezi hilo kwa muda wote wa siku nne ili watoto wapate chanjo hiyo.
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa