Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dkt. Khalfan Haule amethibitisha kufariki kwa wagonjwa saba wa kipindupindu katika Wilaya ya Sumbawanga huku wagonjwa wengine 44 wakibaki wodini kuendelea kupatiwa matibabu na wagonjwa 115 wakiruhusiwa kurudi nyumbani.
Amesema kuwa ugonjwa huo umelipuka tarehe 6 Mei, 2018 katika Kijiji cha Mayenje, kata ya Milepa katika bonde la ziwa Rukwa na kusambaa katika meneo mengine ya Wilaya na hatimae kupatikana kwa wagonjwa wawili katika hospitali ya rufaa ya mkoa.
“Sasa hivi katika bonde la ziwa Rukwa kuna shughuli za uvunaji wa mpunga na hivyo watu wengi hutokea huku juu kwenda bondeni kutafuta vibarua vya kuvuna mpunga kwenye maeneo hayo yaliyoathirika na kipindupindu, maji yanayotumika huko ni machafu kutoka katika madimbi na mito nawaomba viongozi wa dini watoe tahadhari kwa waumini hasa katika maeneo yale yalioathirika zaidi,” Alisema.
Alisema hayo alipopewa nafasi ya kutoa taarifa hiyo ya ugonjwa wa kipindupindu na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo wakati wa Mkutano uliowakutanisha wadau wa afya Mkoani hapa kwaajili ya kuzungumzia tahadhari ya ugonjwa wa Ebola uliopo katika nchi ya jirani ya Kongo.
Kwa upande wake Mh. Wangabo alisema kuwa elimu ya tahadhari itatolewa kwa wananchi kupitia mikutano mbalimbali ya hadhara ya wakuu wa wilaya, madiwani pamoja na wakurugenzi ili ifikie hatua ya kusema “kipindupindu sasa basi”.
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa