Idara ya Afya mkoani Rukwa inakusudia kupanua wigo wa utoaji chanjo ya ugonjwa Uviko-19 kwa kuanza kutoa huduma mkoba ili kuwafikia wananchi wengi zaidi waishio vijijini ambao wanakabiliwa na ugumu wa kuvifikia vituo 11 vilivyoainishwa awali kutoa huduma hiyo.
Mganga Mkuu wa mkoa wa Rukwa Dkt.Boniface Kasululu amesema kuwa hatua hiyo imechukuliwa baada ya kubaini kuwa wananchi wengi wanaonesha mwitikio wa kutaka kupata chanjo hiyo inawalazimu kusogeza huduma hiyo maeneo ya karibu na wananchi kutokana Jiografia ya mkoa wa Rukwa ambapo hadi sasa zaidi ya wananchi Elfu Moja wamejitokeza kuchanjwa ndani ya siku tatu tangia kuzinduliwa kwa zoezi hilo.
"Mazingira ya mkoa wa Rukwa ni tofauti na mikoa mingine ambayo baadhi ya wananchi inagua vigumu kufika kwenye vituo ambavyo vimeainisha kutoa chanjo, hivyo lazima tuwasogezee huduma kwenye maeneo yao ya karibu". Alisema Dkt.Kasululu.
Dkt. Kasululu amesema jumla ya wananchi 1,081 tayari wamejitokeza kuchanjwa katika siku tatu tu tangia kuanzishwa kwa zoezi hilo, hali inayoonesha kuwa kuna mwitikio mzuri ambapo takwimu hizo ni wastani watu 300 hadi 350 kwa siku wanaojitokeza kuchanjwa.
Mganga huyo wa mkoa wa Rukwa amesema baada ya huduma kupelekwa karibu vituo vya Afya na Zahanati za karibu wananchi wanatakiwa kwenda kujiorodhesha kwenye vituo hivyo na taarifa itatolewa kwenye timu za chanjo cha wilaya ambapo Wataalamu hao wa afya watapanga siku ya kwenda kutoa huduma kwa makundi ya watu waliojiandikisha kwenye eneo lao.
Mkoa wa Rukwa umepatiwa jumla ya dozi Elfu Ishirini za chanjo hiyo na kwa mujibu wa Dkt.Kasululu iwapo mkakati huo wa huduma mkoba utafanikiwa basi wanatarajia kukamilisha zoezi hilo ndani ya mwezi mmoja.
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa