Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amewapongeza walimu wakuu wa shule za msingi zilizopo manispaa ya Sumbawanga kwa kufaulisha kwa asilimia 84 katika matokeo ya darasa la saba kwa mwaka 2017.
Amesema kuwa kwa kufanya hivyo wameteeleza Ilani ya Chama cha CCM ambayo ndio inayoongoza serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Uongozi wa Rais Dk. John Pombe Magufuli, ilani hiyo inaeleza ufaulu wa zaidi ya asilimia 80 kwa shule za msingi ili kuweza uwakomboa wananchi.
Mbali na hayo Mh. Wangabo aliwasisitiza walimu kuwa wanamchango mkubwa katika ufaulu wa mwananfunzi huku wao wakiwa kama “software” na miundombinu kama madawati, majengo na vitabu ikuchukua nafasi katika kukamilisha asilimia 100 za ufaulu wa mwanafunzi.
“Mchango wa walimu katika kumfanya mtoto afaulu ni asilimia 55 na asilimia 45 ni miundombinu kama vitabu, majengo na madawati, walimu mkifanya kazi vizuri na wathibiti ubora wa elimu ambao kwa pamoja ni kama “software” basi elimu itakuwa bora sana,”
Amesema hayo alipokuwa akiongea na walimu wakuu kutoka katika shule za msingi 67 za serikali na binafsi waliokutana kwaajili ya kujadili namna ya kuboresha ufaulu katika Manispaa ya Sumbawanga, Halmashauri ambayo inabeba sura ya Mkoa.
Katika kusisitiza uwajibikaji kwa walimu hao wakuu Mh. Wangabo amewataka kutojihusisha na michango ya aina yoyote na kuwa mwenye dhamana ya kuchangisha ni Mkurugenzi wa Halmashauri kwa mujibu wa miongozo iliyopo.
Jumbe Is haq ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Istiqaama amepongeza juhudi za serikali katika kuhakikisha wananfunzi wanakuwa na mazingira mazuri ya kujifunzia na kumuomba Mh. Wanagabo kufanya kikao rasmi na walimu wote ili kujua changamoto za walimu hao na kuona namna ya kuzitatua.
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa