Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ameiagiza mamlakaya viwanja vya ndege (TAA) kwa kushirikiana na Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga kuanza hatua za wali za maandalizi ya uwanja wa ndege wa kimataifa unaotarajiwa kujengwa katika Kijiji cha Kisumba kata ya Matanga, Wilaya ya Sumbawanga.
Amesema kuwa kutokana na ufinyu wa eneo la Kiwanja cha Sumbawanga mjini kinachoendelea na taratibu za kuukamilisha ni vyema mamlaka hiyo ikaanza kutafuta hatimiliki ya uwanja wa Kisumba pamoja na kuweka mipaka inayoonekana katika uwanja huo pamoja na kuendelea kuwazuia wananchi kuvamia na kuendelea na ujenzi.
“Hatua za mwanzo za kupata hati ya hicho kiwanja ziendelee ili eneo hilo limilikiwe kisheria japokuwa lilitengwa tangu miaka hiyo kwaajili ya dhumuni hilo, ili muwazuie wananchi kuvamia maana mji unakua, watu wanongezeka na aerdhi haiongezeki, ili kuwazuia watu hilo lianze haraka,” Alisisitiza.
Eneo la Uwanja wa ndege wa Kisumba lenye ukubwa wa ekari 3411 na umbali wa kilomita 19 toka Sumbawanga mjini, lilitengwa tangu kuanzishwa kwa Mkoa wa Rukwa mwaka 1974 ambalo mpaka sasa hakuna mwananchi aliyevamia na kujenga.
Nae Kaimu Meneja wa uwanja wa ndege wa Sumbawanga Musa Mchola ameeleza kuwa Eneo hilo liliwekewa mipaka kwa alama ya bikon baada ya kutengwa kwa madhumuni ya kuanzishwa kwa uwanja wa ndege ambapo hivi alama hizo zimepotea na baadhi ya watu kuingia na kuanza kulima.
“Eneo hilo lilitengwa mwaka 1974 ila sasa hivi kuna baadhi ya wananchi wa vijiji vya jirani wameingia na kuanza kulima ila baada ya kuongea nao wakafanya Mkutano wa vijiji na kuniandikia barua ya kukiri kuwa wamevamia na kuahidi kuwa hadi mwezi June, 2018 watakuwa wamehama,” alibainisha.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa manispaa ya Sumbawanga Hamid Njovu amesema kuwa eneo la uwanja wa ndege uliopo katikati yam ji wa Sumbawanga ni dogo la Ekari 74 ukilinganisha na eneo lililopo Kijiji cha kisumba 3411, jambo lililomsukuma Meneja wa Wakala wa Barabara Mkoa wa Rukwa Mhandisi Msuka Mkina kuongeza kuwa mwaka wa Fedha 2018/2019 kutakuwa na upembuzi yakinifu kwaajili ya kujenga uwanja wa kimataifa wa Kisumba na uliopo wa Sumbawanga utatumika kwa matumizi ya “Domestic”.
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa