Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amewataka wakulima wote mkoani Rukwa kuhakikisha wanayasafisha mahindi yao kabla ya kuyauza ili kupata soko la uhakika na pia kujiepusha na magonjwa mbalimbali ikiwemo kansa endapo mahindi hayo yatauzwa yakiwa na mchanganyiko wa mahindi yaliyooza na takataka.
Amesema kuwa mahindi yaliyooza yana sumu Kuvu ambayo hutengenezwa yakiwa na upepo na unyevu, sumu ambayo huleta kansa kwenye miili ya binadamu endapo mahindi hayo yatasagwa na athari hiyo haitakuwa kwa watanzania peke yao bali hata walaji waliopo nje ya nchi.
“Muhakikishe kwamba mahindi yale mnayoyachambua hambakishi mahindi yaliyooza na matakataka yale mahindi yaliyooza ni sumu ile inaitwa sumu kuvu inakuja kutengenezwa baadae kukiwa na upepo na unyevu na kusababisha kansa, lakini pia mawe yakiingia kwenye mfumo wa kusaga unga, chakula kikiwa na mawe kitasababisha kidole tumbo, ambapo hadi ufanyiwe upasuaji ndipo upone,” Alisema
Na kuongeza kuwa kwa kufanya hivyo kutasaidia kutangaza bidhaa nzuri zitakazo Mkoa wa Rukwa katika mikoa mbalimbali nchini lakini pia kama usafi huo utazingatiwa utaleta sura nzuri katika soko la kimataifa na hatimae kuitangaza nchi kwa bidhaa zake bora.
Ameyasema hayo alipotembelea kiwanda cha kuzalisha unga cha Mbasira Food Industries kilichopo kata ya Malangali, Wilaya ya Sumbawanga kujionea maendeleo ya kiwanda hicho chenye uwezo wa kuzalisha tani 36,000 za unga kwa mwaka na kuongea na vibarua wa kiwanda hicho waliokuwa wakitenga mahindi mazima na mabovu kwaajili ya uzalishaji.
Nae Mkurugenzi wa Mbasira food Industries Ltd Mikidadi Kassanda amesema kuwa changamoto kubwa wanayopambana nayo katika kununua mahindi kutoka kwa wakulima ni kupata machanganyiko wa mahindi mabovu na kusababisha kupoteza kilo nne za mahindi mabovu katika kila kilo 100 za mahindi wanayouziwa na wakulima.
“Moja ya changamoto tunazokumbana nazo ni ukosefu wa mafunzo bora kwa wakulima juu ya uzalishaji bora wa mahindi na hatimae kupata mahindi yasiyo na viwango,” Alisema.
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa