Anaandika Sammy Kisika, Nanenane 2022
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Queen Sendiga ameanza na suala la kutaka kutokomeza Udumavu mkoani Rukwa mara tu baada ya kuonana na Mkuu wa wilaya ya Sumbawanga na Wakurugenzi wa halmashauri za mkoa huo.
Akiwa anawaonana uso kwa uso na Watendaji wa halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga alipotembelea kwenye Banda la Maonesho ya Nanenane kwenye viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya, Mkuu huyo wa mkoa alisema ni aibu kuona mkoa kama Rukwa unaripotiwa kuwa na udumavu kwa watoto.
Alisema”Hii mikoa inasifika kwa uzalishaji wa vyakula vingi, lakini unaambiwa kuwa udumavu umezidi, hii inanishangaza sana, ebu tufanye jambo kuondokana na hali hiyo”.
Mkuu huyo wa mkoa ambaye yuko njiani kuelekea kwenye kituo chake kipya cha kazi mkoani Rukwa akitokea mkoani Iringa alisema tatizo linazilozikumba halmashauri nyingi ni kutotekelezwa kwa afua za lishe kulingana na kalenda za Wataalamu wa Idara ya Afya katika halmashauri hizo.
“Ninyi wakubwa mnadhani hizi kazi za masuala ya lishe ni kwaajili ya Manesi pekee yao na watu wao kwenye idara ya Afya, nyie mko bize na mambo mengine, hii sio kweli kwasababu hawa wanaweza kupanga lakini wasipowezeshwa kibajeti haina maana”,alisema
Aidha alishauri kuwa kila halmashauri iandae mpango kazi ili upitishwe na vikao husika na mwisho wa Robo ya bajeti Kamati husika zikae na kufanya tathimini iwapo malengo yaliyopangwa yamefikiwa kwa idadi ya kaya.
Alisema Kamati hizo ziwe na uwezo w kubadili bajeti kulingana na kipaumbele kwa muda huo, kama ni ununuzi wa dawa au kwaajili kuongeza suala la lishe kwenye kaya, badala ya kukaa na mipango ambayo afua zake hazitekelezeki.
Manispaa ya Sumbawanga inasilimia 47 za udumavu kwa watoto waliochini ya umri wa miaka mitano ndani ya halmashauri hiyo.
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa