Mkurugenzi wa Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga amewataka viongozi wote wa vitongoji na mitaa kwenye halmashauri hiyo kuhakikisha wanashiriki shughuli za usafi kwenye maeneo yao ihali wakitambua kuwa huo ni wajibu wao na wananchi kwa ujumla.
Wito huo umetolewa katikati ya wiki hii na Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Bw. Hamid Njovu wakati akizungumza na watendaji, viongozi na wenyeviti wa mitaa na vitongoji mbalimbali katika kikao maalumu kilichofanyika kwenye ukumbi wa Manispaa hiyo.
“Nawaombeni mkawaeleweshe wananchi wetu kupitia vikao mbalimbali ambavyo mtaviitisha kwenye maeneo yenu, watambue kuwa usafi ni jukumu la kila mwananchi ambaye anatakiwa kuhakikisha eneo lake linakuwa safi nje na ndani ya nyumba yake na maeneo ya biashara na hapa niongeze kuwa msiwategee watumishi wa halmashauri kuwa ndio wasimamizi pekee wa zoezi hilo usafi.” Alisema Bw,Njovu
Kwa kuanza Mkurugenzi huyo amewataka viongozi hao kuhakikisha wanachi wao wanajitokeza kwa wingi katika zoezi la usafi la mwisho wa mwezi huu maarufu kama ‘Magufuli Day’ ili kuhakikisha mazingira ya mji wa Sumbawanga yanakuwa ya kuvutia kutokana usafi wa uhakika utaofanyika safari hii.
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa