Ameandika Kisika S.J
Zaidi ya migogori 200 ya ardhi kwenye maeneo mbalimbali mkoani Rukwa imetatuliwa na Ofisi ya Kamishna Msaidizi wa Ardhi mkoani humo katika kipindi cha mwezi mmoja kutokana na utataribu mpya wa ulioanzishwa wa kuwafuata wananchi kwenye maeneo husika.
Kamishana Msaidizi wa Ardhi wa mkoa huo Swagile Msananga amesema baada ya kutafakari kwa kina ofisi yake imeamua kuja na utaratibu huo wa kumaliza changamoto za ardhi huko huko mitaani kwa kuwafuata wananchi kuwasikiliza na kutatua kero zao.
Swagile alisema utaribu huo huwajumuisha watumishi wote wa ofisi hiyo ambao wanakwenda mitaani kukutana na kuzungumza na wananchi na kwenda kuyatazama maeneo husika kisha kushauriana kwa pamoja na kupata muafaka, iwe ni suala la changamoto za kupata hati za nyumba, mashamba na hata migogoro ya mipaka.
“Unajua wako baadhi ya wananchi kuisogelea ofisi ya serikali kwao huwa ni shida, wanakuwa waoga, hivyo sisi tunakwenda mtaani ili kuwafanya wawe hurunkuzungumza na kuwapa maelekezo muhimu ya namna ya kufanya ili waweze kutatuliwa shida zao kwa haraka.
Aidha Kamishana Msaidizi huyo wa Ardhi mkoa wa Rukwa alisema utaratibu huo unakwenda sanjari na jutoaji wa hati za ardhi huko huko mitaani baada ya wananchi husika kukamilisha taratibu zote za kiserikali juu ya umiliki wa ardhi.
Swagile alisema wameanza zoezi hilo katika Manispaa ya Sumbawanga kwa mitaa ya pembezoni na linaonekana kufurajiwa na wananchi wengi.
Kwa upande wa wananchi wamesema kuwa wanaunga mkoano utaratibu huo na wanaufurahia sana, huku wakiipongeza ofisi ya Kamishna wa ardhi mkoa wa Rukwa kwa kufanya kazi kwa uwazi, haraka na uaminifu katika kuwahudumia wananchi.
Ofisi ya hiyo ya Ardhi licha ya kufanya kazi kwa kushirikiana na Wataalamu wengine wa halmashauri, wanaamini kuwa mpango huo utaondoa changamoto na kesi nyingi za ardhi ambazo wananchi wamekuwa wakihangaika nazo kwa muda mrefu.
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa