Imeandikwa na Sammy Kisika.
Waandishi wa habari na Asasi zisizo za kiserikali Kanda ya Nyanda za Juu Kusini wamesema mabadiliko ya kiutendaji yanayofanyika kwenye ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali CAG yanasaidia kuondoa changamoto za hesabu kwenye Taasisi nyingi za serikali na Mashirika ya umma.
Wakizungumza katika Warsha ya Toleo Maalum kwa wananchi na ukusanyaji wa maoni iliyofanyika mwishoni mwa wiki Jijini Mbeya Waandishi hao walisema kuwa kitendo cha Ofisi ya CAG kukusanya Wataalam wa kada mbalimbali kinaondoa changamoto za ukaguzi na hata maelekezo muhimu yatakayoleta tija kwa Idara mbalimbali za serikali.
Waandishi hao wamesema kuwa kulingana na maelezo yaliyotolewa hivi sasa Ofisi ya CAG ina Wataalam wa TEHAMA, Wahandishi, Wachumi, Wabobevyu wa utawala na wengine wengi hivyo inakuwa rahisi kuweza kushauri halmsahauri na hata idara zinginezo katika kutekeleza miradi yao kwa weledi mkubwa.
Akizungumza kwenye Warsha hiyo Mchumi kutoka ofisi ya CAG Emmanuel Philipo alisema kuwa hivi sasa Ofisi ya CAG imekwishaandaa Mpango Mkakati wa miaka mitano kwa kipindi mwaka 2021 hadi 2026 mpango unakwenda kufanya ukaguzi kwa weledi mkubwa zaidi.
Philipo alisema kwenye Mpango huo Ofisi ya CAG itajikita kufanya ukaguzi wa mahesabu kwa kuzingatia Ufanisi (Performance Audit). Ukaguzi wa Kiufundi (Technicla Audit), Ukaguzi wa Kiuchunguzi (Forensic Audit), Ukaguzi Maalum (Special Audit) na ukaguzi wa Mifumo ya TEHAMA (IT Audit).
Mchumi huyo alisema lengo ni kuhakikisha wanafuatilia matumizi ya fedha za serikali na kushauri namna ya utekelezaji kmiradi lakini pia namna ya kutunza kumbukumbu za kifedha ili kuondoa ongezeko la dosari za kiukaguzi na kuzifanya taasisi nyingi kuwa na hati safi.
"Hii leo CAG anauwezo wa kwenda kufanya ukaguzi mradi ukiwa umeanza kutekelezwa au aukiwa unatekelezwa na akatoa ushauri wa kitaalamu iwapo kuna dosasri amezibaini ziwe za kimahesabu au kiufundi hivyo hii inasaidia uwezekano wa wahusika kuingia katika hoja zisizo za lazima, ni mfumo bora na wa kisasi kwa Taifa letu." alisema Philipo
Alisema lengo la Mpango Mkakati huo ni kuwa Ofisi ya CAG iwe ni Taasisi ya kuaminika nay a kisasa kwenye ukaguzi wa Umma na inayotoa huduma za ukaguzi wa viwango vya juu zinazoimarisha Imani kwa umma.
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa