Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga imeanzisha utaratibu mpya wa kuazimisha sherehe za maonyesho Wakulima za Nane Nane katika sehemu mbili tofauti.
Sherehe hizo zitafanyika kiwilaya katika eneo la Katumba Azimio katika Manispaa ya Sumbawanga na zile za Kikanda jijini Mbeya.
Kwa mujibu wa Afisa Kilimo wa Manispaa ya Sumbawanga Bw.George Lupilya sherehe zimetenganishwa kuwapa fursa wakulima wa Manispaa ya Sumbawanga kujifunza Teknolojia za kisasa katika kilimo na ufugaji tofauti na awali ambapo kundi la wakulima wachache walikuwa wakipata nafasi ya kushiriki maonyesho ya Nane Nane Kikanda huku wengine wakikosa nafasi.
Bw.Lupilya amesema maonyesho ya Nane Nane kiwilaya yanalenga kuwapa ujuzi wakulima kujifunza mbinu nyingi za kilimo cha kisasa pamoja na ufugaji, na kutoa wito kwa kila Mkulima na vikundi vyao kujiandaa kushiriki maonyesho hayo.
Alisema tayari mchakato wa kuliandaa eneo la Katumba Azimio limeanza na halmashauri inatarajia kukutana na wadau kulingana na makundi yao ili kuendelea kupata mawazo yao na mikakati ya kuboresha sherehe hizo za Nane Nane mwaka huu..
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa