Mwenge wa Uhuru umezindua na kuweka mawe ya msingi katika miradi 13 yenye thamani zaidi ya bilioni 8 katika Manispaa ya Sumbawanga.
Hayo yalisemwa na Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dk. Khalfan Haule wakati akiukabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen.
“Katika Manispaa ya Sumbawanga, Mwenge wa Uhuru ulikimbizwa katika maeneo mbalimbali na kufanya kazi za, Kuzindua, Kufungua, Kuweka mawe ya Msingi na kukagua Miradi yenye jumla ya Shilingi 8,283,067,927.20,” Dk. Khalfan alifafanua.
Miongoni mwa miradi iliyozinduliwa ni pamoja na kiwanda cha kusindika maziwa wenye thamani ya Tsh. 123,698,382 uliopo kata ya Kizwite na mradi wa ujenzi wa Zahanati katika Kijiji cha Luwa wenye thamani Shilingi 172,209,616 uliopo Kata ya Ntendo na Maabara ya Fizikia katika shule ya sekondari Mazwi wenye thmani ya tsh. 38,144,000.
Pamoja na hayo Mwenge wa Uhuru uliweka mawe ya msingi katika miradi kadhaa ikiwemo mradi wa kiwanda cha kujaza Gesi wenye thamani ya Shilingi 750,000,000 uliopo Kata ya Ntendo, Ujenzi wa shule mpya Kashai wenye thamani ya Tsh. 126,480,000 Katika Kata ya Momoka, Mradi wa Viwanja 153 wenye thamani ya Tsh. 600,000,000 katika Kata ya Ntendo na Barabara ya Lami 5 Km yenye thamani ya Tsh. 5,368,689,000 Kata ya Katandala & Majengo
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa