Mwenge wa Uhuru ni Chombo kilichoasisiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mwaka 1961 ikiwa ni tunu na ishara ya kuwepo kwa Taifa huru la Tanganyika. Tangu kuanzishwa kwa mbio hizi, Mwenge wa Uhuru umekua kichocheo kikubwa katika kuimarisha Uhuru wa Nchi, Umoja wa Kitaifa, Kudumisha Amani, kulinda Muungano na kuhamasisha Maendeleo ndani na nje ya Nchi ya yetu.
Mwenge wa Uhuru umekua kichocheo kikubwa kwa Maendeleo katika Halmashauri yetu. Mbio za Mwenge wa Uhuru 2022 katika Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga, utakimbizwa Kilomita 88.8 katika maeneo mbalimbali na utafanya kazi za kuzindua, kukagua, kuweka Mawe ya Msingi na kutoa Mikopo kwa Vikundi. Jumla ya gharama ya Miradi yote ni Shilingi 1,461,109,000
Tunawakaribisha Wakimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa katika Halmashauri yetu ya Manispaa ya Sumbawanga.
Mwenge wa Uhuru ni Chombo kilichoasisiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mwaka 1961 ikiwa ni tunu na ishara ya kuwepo kwa Taifa huru la Tanganyika. Tangu kuanzishwa kwa mbio hizi, Mwenge wa Uhuru umekua kichocheo kikubwa katika kuimarisha Uhuru wa Nchi, Umoja wa Kitaifa, Kudumisha Amani, kulinda Muungano na kuhamasisha Maendeleo ndani na nje ya Nchi ya yetu.
Mwenge wa Uhuru umekua kichocheo kikubwa kwa Maendeleo katika Halmashauri yetu. Mbio za Mwenge wa Uhuru 2022 katika Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga, utakimbizwa Kilomita 88.8 katika maeneo mbalimbali na utafanya kazi za kuzindua, kukagua, kuweka Mawe ya Msingi na kutoa Mikopo kwa Vikundi. Jumla ya gharama ya Miradi yote ni Shilingi 1,461,109,000
Tunawakaribisha Wakimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa katika Halmashauri yetu ya Manispaa ya Sumbawanga.
ORODHA YA MIRADI NA GHARAMA ZA UCHANGIAJI KWA MIRADI ITAKAYOTEMBELEWA NA MBIO ZA MWENGE WA UHURU 2022 KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SUMBAWANGA.
NA |
JINA LA MRADI |
IDARA |
MAHALI MRADI ULIPO |
SHUGHULI |
GHARAMA ZA WACHANGIAJI |
||||
1
|
Mradi wa Vyumba 3 vya Madarasa na Chumba 1 cha Ofisi Shule ya Msingi Kankwale
|
Elimu Msingi
|
Kankwale
|
Kuweka Jiwe la Msingi
|
HALMASHAURI
|
WAHISANI |
WANANCHI |
SERIKALI KUU
|
JUMLA KUU
|
9,894,000 |
|
1,907,000 |
60,000,000 |
71,801,000 |
|||||
2
|
Utoaji wa Mikopo ya 10%
|
Maendeleo ya Jamii
|
Mazwi
|
Kukabidhi mkopo
|
10,000,000 |
|
|
|
10,000,000 |
3
|
Mradi wa barabara Tawaqal Petrol Station -High Court
|
TARURA
|
Katandala
|
Kuweka Jiwe la Msingi
|
|
|
|
975,000,000 |
975,000,000 |
4
|
Mradi wa Zahanati Nambogo
|
Afya
|
Nambogo
|
Kukagua
|
25,000,000 |
|
14,308,000 |
54,000,000 |
93,308,000 |
5
|
Mradi wa Ujenzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima
|
Elimu ya Watu Wazima
|
Nambogo
|
Kuweka Jiwe la Msingi
|
|
|
|
315,000,000 |
|
JUMLA KUU
|
44,894,000 |
0 |
16,215,000 |
1,404,000,000 |
1,465,109,000 |
UWEKAJI JIWE LA MSINGI VYUMBA VITATU (03) VYA MADARASA NA OFISI YA WALIMU SHULE YA MSINGI KANKWALE.
JINA LA MRADI.
Ujenzi wa vyumba 03 vya madarasa na Ofisi 01 ya Walimu Shule ya Msingi Kankwale.
TAARIFA FUPI YA MRADI
Shule ya msingi kankwale ni miongoni mwa Shule za Msingi zinazomilikiwa na Serikali yenye darasa la Elimu ya awali hadi darasa la saba, Shule ina jumla ya walimu 15 kati yao ME 12 na KE 03 na Wanafunzi 960 kati yao WAV 458 na WAS 502.
Kutokana na uchakavu wa Miundombinu ya Shule Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) ilitoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 03 vya Madarasa na Ofisi moja ya Walimu.
UTEKELEZAJI WA MRADI.
Mradi ulipata fedha kutoka Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) kiasi cha Tsh. 60,000,000/= (Milioni sitini tu) iliyoingia tarehe 27/12/2021 baada ya mapokezi ya fedha ujenzi ulianza kwa mfumo wa “Force account” hadi sasa ujenzi unendelea.
GHARAMA YA MRADI.
WACHANGIAJI:-
Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) 60,000,000
HALMASHAURI: 9,894,000
WANANCHI: 1,907,000
MATUMIZI: 71,801,000
SALIO: 0
TAREHE YA KUANZA MRADI: 21/02/2022
TAREHE YA KUMALIZA MRADI: 21/07/2022
MANUFAA YA MRADI
Kuondoa uchakavu wa vyumba vya Madarasa uliokithiri katika miundombinu ya Shule kwa muda mrefu na kuongeza ubora wa mazingira ya kujifunzia na kufundishia. Ndugu Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, tunaomba uweke jiwe la Msingi ujenzi wa vyumba 03 vya Madarasa na Ofisi 01 ya Walimu Shule ya Msingi Kankwale.
TAARIFA YA KUKABIDHI MKOPO KWA KIKUNDI CHA VIJANA.
TAARIFA FUPI YA MRADI.
Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga inaendelea kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya 2020/25 kwa kuhakikisha inatoa mikopo kwa vikundi mbalimbali vya Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu ili waweze kujikwamua kiuchumi na kuendesha maisha kwa ujumla, hii inafanyika kwa kutoa mikopo ya 10% kutoka mapato ya ndani kwa Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu. Lengo kuu ni kuvijengea uwezo wa kujitegemea na kutoa ajira kwa makundi hayo kupitia sekta binafsi.
TAARIFA YA UTEKELEZAJI.
Kwa mwaka wa fedha 2022/23 Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga imetenga kiasi cha shilingi 184,450,900/= kwa ajili ya kutoa mikopo kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu. Halmashauri inatoa kiasi cha mkopo wenye thamani Tsh 10,000,000/= kwa kikundi cha Vijana chenye wanachama 5 Mkopo huu ni sehemu ya Mikopo ya Robo ya kwanza ya Mwaka wa Fedha 2022/2023.
GHARAMA: 10,000,000
WACHANGIAJI:-
HALMASHAURI: 10,000,000
MCHANGANUO WA MKOPO WA:
Vijana: 10,000,000
TAREHE YA KUANZA MRADI: 21/09/2022
TAREHE YA KUKAMILIKA MRADI: Endelevu
MANUFAA YA MRADI:
UWEKAJI WA JIWE LA MSINGI KATIKA BARABARA YA TAWAQAL PETROL STATION – HIGH COURT YENYE UREFU WA KM 2.03 ILIYOJENGWA KWA KIWANGO CHA LAMI TARURA MANISPAA YA SUMBAWANGA.
JINA LA MRADI: Ujenzi wa kiwango cha Lami Barabara ya Tawaqal Petrol Station – High Court yenye urefu wa Km 2.03.
TAARIFA FUPI YA MRADI
TARURA Manispaa ya Sumbawanga inajumla ya km 476.34 kati ya kilometa zota, kilometa zilizojengwa kwa kiwano cha Lami ni 31.19, kilometa zilizojengwa kwa kiwango cha Changarawe ni 121.71 na kilometa 324.44 ziko katika hali ya udongo.
Katika mwaka wa fedha 2021/2022 Serikali ilitoa fedha kiasi cha Tshs 500,000,000 zilizotokana na Makusanyo ya Tozo na kiasi cha Tshs 500,000,000 kutoka mfuko Mkuu wa Serikali (Jimbo). Fedha hizo zilitumika katika ujenzi wa Barabara yenye urefu wa kilometa 2.03 kwa kiwango cha Lami nyepesi aina ya Double Surface Dressing (DSD).
Kazi zilizofanyika ni kufanya usafi, kukata na kuondoa tabaka la udongo dhaifu, ujenzi wa tabaka la kwanza la changarawe aina ya G7 lenye unene wa mm 200, ujenzi wa tabaka la pili kwa changarawe aina G15 kwa unene wa mm150, ujenzi wa tabaka la tatu kwa changarawe aina G45 kwa unene wa 150mm na ujenzi wa tabaka nne kwa mchanganyiko wa kokoto aina ya CRR kwa unene wa mm150.
Pia barabara hii imemaliziwa juu kwa kutumia kokoto zenye ukubwa wa mm20 na mm10 zilizowekwa na kushindiliwa juu ya Lami.
MAPOKEZI YA FEDHA NA UTEKELEZAJI WA MRADI.
Mradi huu ulitekelezwa kwa awamu mbili tofaouti kwa kutumia mkandarasi mmoja aitwaye M/S SUMRY ENTERPRISE LTD wa Sumbawanga.
Awamu ya Kwanza.
Ujenzi wa Km 1.0 Mkataba Na.AE/092/2021-2022/RKW/W/35 kuanzia Barabara kuu hadi Mahakama kuu kwa kutumia chanzo cha fedha kutoka Mfuko Mkuu wa Majimbo.
Mradi huu ulianza tarehe 01/09/2021 na kukamilika tarehe 28/02/2022 kwa gharama ya Tshs 475,000,000.00.
Fedha iliyopokelewa na kulipwa kwa Mkandarasi mpaka sasa ni kiasi cha Tshs 467,271,052.
Awamu ya Pili.
Ujenzi wa Km 1.030 Mkataba Na.AE/092/2021-2022/RKW/W/51 kuanzia Mahakama kuu hadi Barabara ya Mwaiseni – Kanisa la Neema kwa kutumia chanzo cha fedha zinazotokana na Makusanyo ya Tozo za Mafuta.
Mradi huu ulianza tarehe 08/11/2021 na kukamilika tarehe 29/04/2022 kwa gharama ya Tshs 499,822,820.00
Fedha zilizopokelewa na kulipwa kwa Mkandarasi ni kiasi cha Tshs 403,099,487.83
MANUFAA YA MRADI
Baada ya kukamilika kwa barabara hii imerahisisha shughuli mbali mbali za usafiri na usafirishaji pamoja na kuongeza kuboresha Mji wa Manispaa ya Sumbawanga. Pia kukamilika kwa barabara hii imepunguza sana uwezekano wa kuharibika kwa vyombo vya moto hasa Magari, Bajaji na piki piki kutokana na hali halisi ya barabara ilivyokuwa awali.
JINA LA MRADI: Klabu ya kupambana na Ukimwi, Rushwa, Dawa za Kulevywa na Elimu ya Lishe
TAARIFA FUPI YA MRADI
Shule ya sekondari Kizwite ni miongoni mwa shule za sekondari zinazomilikiwa na Serikali yenye kidato cha kwanza mpaka cha sita, Shule ina jumla ya wanafunzi 1764. Aidha, kwa upande wa walimu, shule inajumla ya walimu 53 kwa mchanganuo wa Me 30 na Ke 23.
IDADI YA WANA KLABU: 60
IDADI YA WAWEZESHAJI/WAKUFUNZI WA KLABU: 5
TAREHE YA KUANZA MRADI: 06/11/2011
TAREHE YA KUMALIZA: Endelevu.
MANUFAA YA MRADI:
Vijana kupata Elimu ya magonjwa ya kujamiiana pamoja na maambukizi ya virusi vya UKIMWI na njia za kujikinga.
Vijana kupata uelewa juu ya athari za unyanyapaa kwa watu waishio na maambukizi ya VVU na UKIMWI mashuleni na katika jamii watokazo.
Kujenga uelewa mzuri unaoridhisha kwa wanafunzi juu ya maswala ya UKIMWI, na Dawa za kulevya.
Kundi la Vijana hususa ni walio mashuleni Kupata elimu juu ya madawa ya kulevya na madhara yake kwao na kwa Taifa zima.
Vijana walio mashuleni kuona umuhimu wa kuwafikia vijana wengine wote katika jamii inayotuzunguka na kujadili juu ya athari za kujiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya na athari zake katika Taifa.
Mradi huu umekuwa chachu kwa vijana kujitambua kwa kujua umuhimu wao kwa Taifa hivo kuichukua elimu hii kama endelevu na inayopaswa kurithishwa kidato mpaka kidato na jamii hususa ni katika kundi rika linalotuzunguka.
Vijana kupata mbinu mbalimbali za utoaji taarifa kwa vyombo vya usalama endapo itabainika kuna aina ya uhalifu unaohusiana na utumiaji wa dawa za kulevya katika jamii husika.
KUWEKA JIWE LA MSINGI TAASISI YA ELIMU YA WATU WAZIMA
JINA LA MRADI: UJENZI WA MADARASA MANNE, CHUMBA CHA WATOTO, VYOO, NA JENGO LA UTAWALA.
TAARIFA FUPI YA MRADI:
Mkoa wa Rukwa ni miongoni mwa mikoa mitatu inayotekeleza mradi wa SEQUIP, Mradi huu unahusu ujenzi wa kituo cha mafunzo cha waichana walioshindwa kuendelea na masomo ya sekondari kwenye mfumo rasmi kwa changamoto mbalimbali ikiwemo ujauzito.
UTEKELEZAJI WA MRADI
Mradi huu unatekelezwa kwa “Force Account” fedha awamu ya kwanza tarehe 18/02/2022 zilipokelewa Tsh. 150,000,000/= na fedha awamu ya pili tarehe 16/05/2022 zilipokelewa Tsh. 170,000,000/= fedha hizi ni kwa ajili ya ujenzi wa madarasa manne ,chumba cha kulala watoto vyoo pamoja na jengo la utawala.
MAKISIO YA MRADI: 320,000,000
MATUMIZI: 302,743,813.51
SALIO: 17,256,186.49
TAREHE YA KUANZA MRADI: 15/03/2022
TAREHE YA KUMALIZA MRADI: 30/09/2022
MANUFAA YA MRADI:
Mradi huu utakapokamilika utatao fursa ya elimu kwa watoto wa kike waliopata changamoto ya kushindwa kuendelea na masomo katika mfumo rasimi, watu wenye mahitaji ya kielimu kuanzaia wasiojua kusoma, kuandika na kuhesabu na watu wote wenye uhitaji wa kujiendeleza kielimu kuanzia sekondari hadi elimu ya juu.
Maalum za Mwenge wa Uhuru Kitaifa tunaomba umeweka jiwe la Msingi ujenzi wa vyumba viwili (4) vya madarasa, Chumba cha watoto, vyoo na jengo la Utawala vya Taasis ya Elimu ya Watu Wazima vinavyojengwa kwenye eneo la Nambogo mjini Sumbawanga.
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa