Shule zenye Wanafunzi wenye mahitaji maalumu na zile za Elimu Jumuishi mkoani Rukwa kwa kushirikiana zimeshsauriwa kuendelea kutafuta Wahisani ambao watawawezesha wanafunzi hao kusoma kwa kutumia nyenzo zenye teknoloji za kisasa na kuweza kufanya vizuri katika masomo yao.
Ushauri huo umetolewa na Katibu Tawala Msaidizi wa mkoa wa Rukwa Samson Hango wakati akikabidhi msaada wa mashine maalumu za kusomea Orbit Reader 20 vyenye thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni 42 kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu wa Shule ya Sekondari Kantalamba.
Mashine hizo zimekabidhiwa kwa Wanafunzi 22 zilizotolewa na Shirika Kilimanjaro Blind Trust Africa lenye makao makuu nchini Kenya, ambapo vifaa vyote vinathamsni ya takribani Shilingi Milioni 42.
Akizungumzia vifaa hivyo Mkuu wa Shule ya Sekondari Kantalamba William Mbelwa alisema Wanafunzi wake watanufaka zaidi na msaada huo kwasababu mashine hizo zimepakiwa mfumo wa vitabu vyote vya sekondari kuanzia Kidato cha Kwanza hadi cha Nne, lakini pia inasaidia katika mawasiliano ya mwanafunzi asiyeona na kiziwi.
Aidha Mbelwa aliwashukuru Wahisani hao kwa msaada huo na akaipongeza serikali kwa kushirikiana na wadau kwa misaada mbalimbali inayotolewa shuleni hapo.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga Samson Medda aliwataka wanafunzi wa shule hiyo kusoma kwa bidii ili kiuweza kufanya vizuri kwenye mitihani yao ya mwisho na kuongeza kuwa hawana sababu ya kufeli kwasababu serikali imeboresha miundombinu ya shule hiyo kwa sasa.
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa