Msanii wa muziki wa kizazi kipya wa mji nwa Sumbawanga Martin Gondwe ama kwa jina la kisanii Tigan Tozi amefikisha kilio cha kushindwa kuendelea na masomo yake ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga Bw. Jacob Mtalinya ili aweze kusaidiwa.
Kilio hicho alikifikisha katika uzinduzi wa filamu ya “Hidden Image” (Taswira iliyojificha) uliofanywa na kikundi cha Great Mind Association (GMA) ambapo mgeni rasmi wa sherehe hizo alikuwa Mkurugenzi wa Manispaa na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa Sanaa wa mji wa Sumbawanga.
“Kubwa niweze kusoma nikiwa nasubiria mirathi, chuo ada yangu ni shilingi milioni 1.5, sehemu ya kukaa ni shilingi laki 2.5 kwa “semester” moja inamaana kwa “semester” mbili ni shilingi laki 5,” Alisema.
Bw. Mtalitinya baada ya kuguswa na kilio cha msanii huyo aliitisha harambee ya kuchangisha kiasi cha Shilingi milioni 2 kutoka kwa wadu hao wa Sanaa waliofika katika uzinduzi huo ili kumuwezesha msanii huyo aendelee na masomo yake wakati akisubiri mirathi baada ya kufiwa na baba yake mzazi mwaka huu.
” Tufanye mawasiliano, tuongezee kwenye hizo ili mwaka huu asiahirishe tuzungumzie mwakani, ombi langu ni kwamba ukatutendee haki, Mwalimu Nyerere alisema kama umetumwa na kijiji wakauza mali zao ukapelekwa kule ili uje uwakomboe halafu tena ukaharibu we unastahili kunyongwa,”
Katika Harambee hiyo ilipatikana kiasi cha Shilingi 800,000/= fedha taslimu ambayo ilichangwa na wadau hao na Bw. Mtalitinya aliongezea iliyobaki na kutimia shilingi mlioni 2 ili msanii huyo aweze kuendelea na masomo.
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa