Mkoa wa Rukwa unaanza kukimbiza Mwenge wa Uhuru hii leo katika wilaya zake tatu ambapo jumla ya miradi 18 yenye thamani ya Shilingi Bilioni 10.5 inatarajiwa kuwekewa Mawe ya msingi na kukaguliwa.
Akizungumza wakati wa mapokezi ya Mwenge huo ukitokea katika mkoa wa Songwe, makabidhiano yaliyofanyika kwenye kijiji cha Tunko wilayani Sumbawanga, Mkuu wa mkoa wa Rukwa Joseph Mkirikiti alisema katika gharama hiyo ya wananchi wamechangia Shilingi Milioni 101.4 sawa asilimia 0.9, huku halmashauri zikichangia Shilingi Milioni 183.094, wakati Wahisani wakichangia Shilingi 286.17 ambazo ni sawa na asilimia 2.7, huku serikali kuu ikichangia Shilingi Bilioni Bilioni 9.9 ikiwa ni sawa na asilimia 94.5
Akizungumzia ujumbe wa Mwenge huo mwaka huu, Mkuu wa mkoa wa Rukwa amesema ujumbe wa Mwenge unasisitiza umuhimu wa matumizi sahihi ya TEHAMA ambayo imesaidi ongezeko laa ukusanyaji wa mapato kutoka Shilingi Bilioni 5 hadi 8 kwa kupitia mifumo maalumu ya ukusanyaji wa mapato kwenye halmashauri zote za mkoa wa Rukwa.
Alisema mkoa wa Rukwa ina mifumo ya TEHAMA ipatayo 32 ambayo ipo kwenye taasisi mbalimbali ikiwa kwenye sekta ya utawala, Afya na Elimu ndani ya halmashauri zote nne.
Mkirikiti alisema mifumo ya TEHAMA inatumiwa na Taasisi na Wakala za serikali kama vile RUWASA,TEMESA,TANROADS,TRA,TANESCO na TARURA ambayo inachochea maendeleo ya mkoa na Taifa kwa ujumla.
Kuhusu mapambano dhidi ya Rushwa Mkuu wa mkoa wa Rukwa alisema katika kipindi cha Juni 2020 hadi Julai 2021 jumla ya malalamiko 269 yaliripotiwa TAKUKURU, ambapo kati ya hayo 102 hayahusiani na rushwa, ikiwa watuhumiwa 15 wamefikishwa mahakamani.
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa