Serikali mkoani Rukwa imewataka Wakandarasi wanaofanya kazi za ujenzi wa barabara watakazozipata kutokana zabuni za Wakala wa barabara wa Mjini na Vijijini (TARURA) kuhakikisha wanaotoa ajira kwa makundi ya vijana na wanawake ambako miradi hiyo inapita.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Katibu Tawala wa mkoa wa Rukwa Benard Makali wakati kikao cha ufunguzi wa makabidhiano ya mikataba ya ujenzi wa barabara zinazojengwa na TARURA katika mkoa wa Rukwa.
Katika kikao hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa RDC mjini Sumbawanga, Mkuu wa mkoa wa Rukwa alisema kuwa iko haja ya miradi ya TARURA kuwanufaisha watu wanaoishi kando ya barabara zinajengwa ili kuyafanya makundi ya vijana na wanawake kupata fursa ya kuiongea vipato na kuinua uchumi wao.
“Utakuta barabara inajengwa eneo fulani au mtaa fulani, lakini wanaopata ajira hapo wanatoka kwenye mikoa mingine tena mbali na eneo husika, hii haipendezi. Tunataka vijana hawa wapate kazi kwenye maeneo yao na suio vinginevyo”. Alisema Mh. Joachim Wangabo
Alisema ujenzi wa miradi hiyo ambayo inawasahau wananchi wa maeneo husika licha ya kuwanyima fursa lakini pia imekuwa ikileta manung’uniko mengi iwapo wanakosa fursa. Aliongeza kuwa zipo kazi nyingi ambao hazihitaji wataalamu kutoka mbali na zinaweza kufanya vijana wa maeneio husika.
Mratibu wa TARURA mkoani Rukwa Injinia Wilson Charles alisema jumla ya miradi yenye thamani ya zaidi ya Shilingi 2.8 itatekelezwa mkoani Rukwa ambapo Wandarasi 12 mkoani humu watapewa fursa ya kufanya kazi hizo huku wengine wakitoka nje ya mkoa wa Rukwa.
Injia Charles alizitaja kazi zinazotarajiwa kufanyika na TARURA ni pamoja na ujenzi wa barabara ya lami yenye urefu wa kilometa 1.0 inayotarajiwa kujengwa kwenye mji mdogo wa Namanyere wilayani Nkasi, ujenzi wa barabara kwa kiwango cha changarawe, kiwango cha udongo na ukarabati wa barabara mbalimbali.
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa