Wataalamu wa kilimo hapa nchini wametakiwa kushirikiana na wakulima katika kuhakikisha elimu na mafunzo yanayotolewa kwenye Maonesho ya Nane Nane yanahawawilishwa na kupelekwa vijiji kwa wakulimambao hawajapata fursa ya kufika kwenye Nane Nane.
Akizungumza katika Ufunguzi wa Manonesho ya Nane Nane 2019 kwenye uwanja wa John Mwakangale Jijini Mbeya, Mgeni Rasmi Naibu Waziri TAMISEMI Mh.Mwita Waitara amesema baada ya kutembelea mabanda mengi kwenye uwanja huo amebaini kuna ubunifu na utaalamu mkubwa uliopo kwenye sekta ya kilimo na mifugo lakini bado hauwanufaishi wakulima na wafugaji walio.
Mh.Waitara amesema halmashauri na wajasiriamali wengi wameweka vitu mbalimbali kwenye maenesho hayo, lakini anapata mashaka iwapo maarifa hayo yanatumika ipaswavyo katika kuhakikisha wakulima wanalima kwa tija huko walipo hususan maeneo ya vijijini.
“Mambo mnayoyafnya humu ndani ni mazuri kweli kweli lakini nina mashaka kama kweli wakulima wanayafahamu na kuyatumia na kama wapo basi ni wachache sana, naomba mbadiliki ili haya maarifa yafawikie wakulima na wafugaji wetu”.alisema Mh.Waitara.
Aidha Naibu Waziri amewataka Wataalamu wa kilimo kufanya tafiti chanya amnbazo zitaleta mapinduzi kwenye kilimo na kuifanya nchi kufikia malengo ya uchumi wa viwanda.
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa