Mstahiki Meya wa Manispaa ya Sumbawanga Mh. Justin Malisawa amesikitishwa na ufinyu wa bajeti ya Wakala wa barabara Mijini na Vijiji (TARURA) iliyotengwa kwaajili ya ujenzi wa barabra inayolelekea katika Kijiji ca Wipanga na Kankwale.
Alisema kuwa wakati kukiwa umebaki mwezi mmoja kuupokea mwenge kuna mradi wa Zahanati ambapo manispaa ya Sumbawanga unataria mwenge ukazindue lakini hali ya barabara ya kuelekea huko si nzuri kiasi wanahofia mwenge usiweze kufika na kuwakosesha wananchi wa Kijiji hicho raha ya kuupokea mwenge.
“Kama sisi wote ni watanzania nataka niliseme hili Mwenyekiti na kama kuna mjumbe anabisha hapa tuweze kuondoka wote mimi wewe na timu hii tuseme kwamba tunafika katika Kijiji cha Kankwale, tuende barabara ya Wipanga; Senga – Sido – Wipanga, Mwenyekiti tukienda kule tukifika wote salama, mimi ninauwezo wa kuja kusimamisha shilingi hapa. Ninachotaka kusema kwa mwaka huu wa 2018/2019 tumepoteza kinamama wajawazito wawili na ukiangalia bajeti iliyotengwa huwezi kufanya chochote,” Alisisitiza.
Kwa upande wake Mratibu wa TARURA Mkoa wa Rukwa Mhandisi Boniface Wiliam alisema kuwa changamoto kubwa ni ufinyi wa bajeti hali inayopelekea kutokamilisha ujenzi wa barabara nyingi kwa wakati huku akiela bajeti iliyopangwa kwaajili ya kutengeneza maeneo korofi ya barabara ya Senga – Sido- Wipanga.
“barabara ya Wipanga ina Kilometa 13 na imetengewa shilingi milioni 50 kwa mwaka wa fedha 2018/2019 na pia mwaka wa fedha 2019/2020 imetengewa shilingi milioni 50 ili kurekebisha maeneo korofi ya barabara hiyo,”Aliwasilisha.
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa