Mbunge wa Jimbo la Sumbawanga Mjini Mh.Aeshi Hilaly ameshauri Manispaa hiyo kuanza kujenga majengo mapya kwa zile shule kongwe ili yaweze kuendana na wakati.
Akizungumza mara baada ya mkutano wa Wadau wa Elimu wa Manispaa hiyo Mh.Aeshi alisema kuwa majengo mengi ya shule Kongwe yamechoka jambo ambalo linachangia kushusha morali ya Walimu na wanafunzi.
“Kuna shule zina majengo ambayo yalijengwa hata mimi kabla sijazaliwa ni enzi hizoooo za Mkoloni lakini hadi hii leo bado yapo na tunaendelea kuyakarabati jambo ambalo halileti tija sana kielimu”.
Alisema ukarabati wa shule hizo umekuwa ukigharimu fedha nyingi hivyo ni bora kujenga majengio mapya ambayo yatakwenda na wakati kulingana na shule hizo kukabiliwa na idadi kubwa ya wanafunzi.
Ametolewa mfano wa kuigwa shule amabzo zimeanza kubadilika na kuleta mvuto kwa kujenga majengo mapya ikiwapo Shule ya Msingi Mlanda B , Malagano, Mawenzusi na Isesa ambazo zinaonekana kuwa na mvuto kutokana na majengo hayo mapya.
Aidha Mbunge huyo aliushukuru uongozi wa Taasisi ya Elimu TEA ambao walitoa fedha kwaajili ya ujenzi wa madarasa kwenye Shule za Mlanda B na Malagano.
Hatahivyo Mh.Aeshi alishauri wadau kuendelea kuchangia kujenga madarasa mapya huku wakiunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya Tano katika suala zima la kuboresha elimu hapa nchini.
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa