Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga imeweka mkakati wa kukarabati masoko yaliyopo na kujenga mengine mapya kwa malengo ya kupanua wigo wa mapato wa halmashauri hiyo.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa halmashuri hiyo Jacob James Mtalitinya wakati akizungumza na wananchi wa kata ya Sumbawanga, alipofanya ziara ndogo katika kitongoji cha Kaswepepe mjini Sumbawanga.
Mtalitinya alisema kuwa halmashauri hiyo inatambua kuwapo kwa baadhi ya maeneo yasiyo rasmi yanayotumiwa na wananchi kama masoko na halmashauri imeendelea kuwaaacha kwenye maeneo hayo hadi pale mipango itakapokuwa tayari ya ujenzi wa masoko mengine.
Mkurugenzi huyo alisema ajenda ya mapato ni ajenda muhimu, hivyo kuboreshwa kwa masoko hayo kutaiwezesha halmashauri hiyo kuwa na wigo mpana zaidi wa ukusanyaji wa mapato kutokana ushuru utakatolewa na watumiaji wa masoko hayo.
Alisema hivi sasa wanachoangalia ni uboreshaji wa huduma muhimu katika maeneo hayo yasiyo rasmi kama vile vyoo na mambo mengine hadi pale mkakati huo utakapo kamilika.
Mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa Sumbawanga ameanzisha mkakati wa kuboresha makusanyo ya mapato ya halmashauri hiyo, kutoka kwenye vyanzo mbalimbali vya ndani, kutokana na halmashauri hiyo kuonekana kuwa chini kwa kiwango cha ukasanyaji wa mapato ndani ya mkoa wa Rukwa ukilinganisha na halmashauri zingine, huku pia ikikabiliwa na changamoto za utoaji wa huduma za kijamii kwa wananchi wa Manispaa hiyo.
Sumbawanga Municipal Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 187, Sumbawanga
Simu ya Mezani: +255252802163
Simu ya Kiganjani: +255 735519681/ +255
Barua pepe: md@sumbawangamc.go.tz
HakiMiliki ©2017 Sumbawangamc . Haki Zote Zimehifadhiwa